OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Ili watu wawe huru kutoa mawazo na hisia zao lazima mazingira yawe rafiki. Hata hivyo kuna wakati watu huwa na mazingira yasiyo rafiki kwa kuwa watu wanahitaji mawazo ya namna fulani au yanayosapoti tu. Wakija watu wenye mawazo tofauti hupewa jina la "wabishi". Neno ambalo lina maana ya kwamba siwezi kujibu hoja zako, ila siwezi kuboresha hoja zangu ili ukubali nikisemacho.
Tamaduni hii imeanza kitambo sana tangu watu wakiwa watoto ambapo mtu akiwa anahoji sana huitwa mbishi au mtata. Suala ambalo taratibu huondoa hali ya watu kuwasilisha mawazo yao wakiona haya ya kuitwa majina hayo. Wakati tunazungumzia kuwa na inclusive environment wakati huohuo hatutaki inclusivity kwa kushindwa kukubali hoja tofauti.
Hali hii imekuja hadi sasa watu wanaokosoa badala ya kujibiwa kwa hoja wanajibiwa kwa kupotea. Suala ambalo linazidisha woga kwa wengine huko kijijini.
Madhara ya hii tabia
Moja ya madhara ya mtu kuitwa mbishi ni kuacha kutoa hoja. Maana kama umeanza kwa kuniita mbishi, in no way unaweza kutulia kuchambua hoja. Maeneo mbalimbali baada ya kujua hii, huwa wanashiriki vikao na midahalo wakitoa hoja zinaoendana na watawala na wakiondoka wanaanza kuongea hoja zao halisi.
Hii huathiri zaidi watafiti, NGOs na watendaji wa serikali katika kupata mawazo halisi ya wananchi badala yake wanapata wanavyotaka kuvisikia kisha watu huongea tofauti baadae. Ambapo unakuta mradi unaleta wenyewe wanasema hata hawakuutaka.
Na baadae waserikali wanasema watu hawa hawawezi kujielezea matatizo yao.
Point ya msingi ni kuwa, tunapotaka kutengeneza mazingira rafiki ya watu kujielezea inabidi tuondoe hizi dhana za name calling badala yake kila mwenye hoja tofauti ajibiwe kwa hoja ili kuweka mazingira ya kila mtu kuona yuko huru kusikilizwa.
Nawasilisha.