BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Kuna hili andiko nimelikuta kwa mdau wa sheria anaitwa Na Bashir Yakub ambaye ni WAKILI
=============
Maombi ama Kesi inaweza kutupwa na Mahakama kwa namna moja kati ya mbili.
Inaweza kutupwa katika namna ambayo huwezi kuirudisha tena/kuifungua upya, ama inaweza kutupwa katika namna ambayo unaweza kuirudisha tena/ kuifungua upya.
Kutupwa katika namna ambayo unaweza kuirudisha tena kitaalam huitwa "STRIKE OUT", wakati ile ambayo huwezi kuirudisha tena hutwa kitaalam "DISMISSAL".
Kesi ya wakina Mdee imetupwa katika namna ambayo inaweza kurudishwa tena/kufunguliwa upya "STRIKE OUT".
STRIKE OUT maana yake kuna kitu kimekosewa ambacho kikirekebishwa kesi inarudishwa/kufunguliwa upya.
Maana yake kesi ya msingi ya uhalali wao bungeni haikusikilizwa hata kidogo, bali Mahakama imesikiliza makosa ya kiufundi na ikaamue iitupe kabla ya kusikiliza kesi ya msingi ili wahusika wakayarekebishe hayo makosa wairudishe tena ama waachane nayo, uamuzi ni wao.
Aghalabu, namna ya kuirudisha ni kuwa kama umejiandaa inaweza kutupwa na muda huohuo hata kabla watu hawajatoka Mahakamani au wakingali bado wanashangilia ukairudisha kwa kufungua nyingine hapohapo.
Ni kurekebisha tu makosa na kuanza upya.
Isipokuwa yale mazuio unayokuwa umepata yanakufa na ile iliyotupwa na hivyo huu muda wa katikati ambao hujafungua nyingine unakuwa haupo salama kwa kuwa huna zuio lolote linalokulinda na hivyo lolote laweza kufanyika dhidi yako.
La kufanya ufungue upya haraka na uombe zuio jingine jipya haraka kabla hujapata madhara ya kutokuwa na zuio.
Kwa msingi huu si ajabu kusikia kesi hii iko Mahakamani upya.
Basi waandishi watusaidie kuwa wanaripoti ilivyo fasaha.
Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.