GE2025 Wakili Ambindwile ajitosa rasmi achukua fomu ya ubunge Iringa Mjini

GE2025 Wakili Ambindwile ajitosa rasmi achukua fomu ya ubunge Iringa Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Ambindwile ambaye ni mtaalamu wa sheria mwenye uzoefu mpana, ambaye pia ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni ya sheria ya The Icon Law Corporate Attorneys, yenye makao yake makuu katika jengo la Law House, Mkoani Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu, Ambindwile amesema: “Nimejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya chama changu. Nia yangu ni kuliwakilisha Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM. Maelezo zaidi nitayatoa baada ya hatua ya upendekezaji wa majina kukamilika.”

, Wakili Ambindwile anashikilia nyadhifa mbalimbali za kitaaluma na kijamii. Kwa sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa Kanda ya Iringa na Njombe, Mshauri wa Masuala ya Kodi aliyeidhinishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na pia Katibu wa Umoja wa Washauri wa Kodi wa Mkoa wa Iringa ambalo ni jukwaa linalowakutanisha wataalamu wa kodi kwa ajili ya kutoa elimu, kubadilishana uzoefu na kusaidia serikali katika kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato.

Katika masuala ya heshima na mila, Ambindwile anajulikana pia kama wakili binafsi wa Mtwa wa Wahehe, Adam Mkwawa wa Pili, nafasi ya heshima kubwa inayotambuliwa na jamii ya Kabila la Wahehe mkoani Iringa.

Mbali na hayo, Ambindwile aliwahi kuhudumu ndani ya Mahakama ya Tanzania kama Mshauri na Msaidizi wa Majaji wa Mahakama Kuu. Ni mjumbe wa bodi kadhaa na ni miongoni mwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi wa bodi kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT).

Mwaka 2023, alitambulika kitaifa baada ya kuongoza jopo la mawakili wa TLS Kanda ya Iringa na Njombe katika kumtetea mjane Maria Ngoda, aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 22 kwa kupatikana na vipande 12 vya nyama ya swala. Kupitia jitihada zao na rufaa iliyowasilishwa Mahakama Kuu, Jaji Mugeta alibatilisha hukumu hiyo, na mjane huyo aliachiliwa huru ikiwa ni tukio lililotajwa kama mfano wa haki na utetezi wa watu wasio na uwezo.

 
Back
Top Bottom