Wakili Bashir Yakub: Kisheria sio kosa mtu kuchoma mali yake

ila jamani kwa hawa wachungaji na manabii wa zama hizi ni wa kuwa nao makini maana wanatafuta upako au hamjui kuwa dini ni biashara siku hizi ya kuingiza mabilioni ya pesa ndani ya muda mfupi..ww unapewa gari unafurahia lakini nyuma ya pazia kuna jambo maalum na pengine jamaa aliyechoma gari labda anamjua vizuri huyo mchungaji wake na mambo yake ya sirini wanajuana hao..sie tunalaani mitandaoni kumbe wahusika wana yao chini ya kapeti..watu wanaoneka wema machoni lakini ndani ni watu na siri zao ni wengine kabisa ogopa sana
 
Iko Mirembe siyo? Maliza Kwanza matibabu
 
Dhumuni la kichoma ndo shida, mbona magari yanachomwa mchana kweupe watengeneza filament na content creators. Huyo amezua taharuki
 
Mkuu umekula kweli mchana? Kwani lazima kutoa zawadi?
Tatizo watanzania mnawaza ulaji zaidi kuliko uhalisia. Kwa hiyo unataka tupokee matukio ya kisanii bila hata kuhoji? Kichwa changu sibebi nywele pekee mnyampaa!
 
Katika muktadha wa Tanzania, kuchoma gari lako mwenyewe kunaweza kuhusisha masuala kadhaa ya kisheria. Ingawa umiliki wa mali binafsi unalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 24(1), ambayo inasema kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria , hii haimaanishi kuwa mmiliki anaweza kufanya lolote na mali hiyo bila kujali sheria nyingine.

Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 (Penal Code, Cap 16) inaeleza makosa yanayohusiana na uchomaji moto kwa makusudi (arson). Kifungu cha 319 kinafafanua kuwa ni kosa la jinai kuchoma moto mali yoyote, ikiwa ni pamoja na mali yako mwenyewe, endapo kitendo hicho kinaweza kuhatarisha maisha ya watu wengine au mali zao.

Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 (Environmental Management Act, 2004) inakataza uchafuzi wa mazingira kwa njia yoyote ile. Kuchoma gari kunaweza kusababisha utoaji wa gesi hatarishi na uchafuzi mwingine wa mazingira, hivyo kuvunja sheria hii.

Sheria ya Bima (Insurance Act) inahusisha makosa ya udanganyifu, ambapo kama mmiliki wa gari atachoma gari lake kwa makusudi ili kudai fidia kutoka kwa kampuni ya bima, kitendo hicho kitachukuliwa kama udanganyifu na ni kosa la jinai.

Kwa kuzingatia haya, ni muhimu kutafuta njia mbadala na salama za kuondoa gari ambalo halitumiki, kama vile kuuza kwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu au kufuata taratibu rasmi za kisheria za uteketezaji wa magari. Hii itakusaidia kuepuka matatizo ya kisheria na kulinda mazingira pamoja na usalama wa jamii inayokuzunguka.

Kuchoma gari lako mwenyewe kunaweza pia kuhusishwa na makosa mengine, kutegemea mazingira ya tukio. Hapa kuna makosa mengine yanayoweza kufuatia:

1. Kuchochea Moto kwa Makusudi: Hili ni kosa la jinai linalotokana na kuchoma moto mali yoyote, hata ikiwa ni ya kwako, ikiwa moto huo unaweza kuathiri usalama wa wengine au mali zao.


2. Kuhatarisha Usalama wa Umma: Ikiwa kitendo hicho kinahatarisha maisha ya watu, kama vile kusababisha mlipuko, moshi hatari, au ajali za moto, hilo linaweza kuhesabika kama kosa la kuhatarisha usalama wa umma.


3. Uvunjaji wa Sheria za Mazingira: Gari lina vipengele kama plastiki, mafuta, na betri ambazo zikichomwa hutengeneza taka hatarishi, hivyo kuvunja sheria za hifadhi ya mazingira.


4. Uharibifu wa Miundombinu ya Umma: Ikiwa gari limechomwa karibu na barabara, majengo, au miundombinu mingine, moto unaweza kuenea na kusababisha uharibifu wa mali ya umma, jambo linaloweza kupelekea kushtakiwa.


5. Uchafuzi wa Hewa: Katika baadhi ya maeneo, sheria za kudhibiti uchafuzi wa hewa zinaweza kuzuia vitendo kama hivyo.


6. Kuzua Hofu au Taharuki: Tukio la moto linaweza kusababisha taharuki miongoni mwa watu waliopo karibu, na katika baadhi ya maeneo, hili linaweza kuhesabika kama kosa la jinai.
 
...Hata kama alipewa Zawadi, na hakununua Kwa Pesa' yake ? Yule aliyempa Zawadi je ,??...
 
Upo sahihi Yakub kuna mwanasheria mmoja pale Arusha amekurupuka kweli bila kujiridhisha akataja kifungu cha 319 cha sheria ya Kanuni ya adhabu. Tena yupo public hatare sana
 
Mkuu vipi kuhusu yule jamaa wa Kigamboni aliyemchoma mke wake kwa mkaa anaweza kuachiwa huru?
 
Wewe ni noma
 
Asante sana
Tunatamani kuona maandiko mengi ya kisheria ,ili watu tujifunze zaidi kutoka kwako.
 
Asante wakili msomi.
Ni jana tu nimetoka kuchoma Boxer zangu zilizochoka.
Basi sina kesi na jamhuri
 
Mkuu,
Kwaio nikitaka kuchoma pesa zangu nilizo zitolea jasho siwezi kushughulikiwa..

Yaan nichukue pesa nachukua kibiriti naanza kuzichoma moto.

Ufafanuzi.
Tutakushughulikia kisawasawa pesa sio yako hata km umehifadhi bank
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…