Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 96
- 1,745
SIO KOSA MTU KUCHOMA MALI YAKE.
Bashir Yakub, WAKILI
+255714047241
MOSI, ili tukio liwe kosa lazima kuwe na upande ambao umeumizwa/ umekosewa(offended party).
Ukimpiga mtu, ukiiba mali ya mtu, ukichoma ama kuharibu mali ya mtu, anayekuwa amekosewa/ ameumizwa ni huyo mwenye mali yake au huyo uliyemdhuru.
PILI, kosa laziwe liwe na mlalamikaji/mshitaki. Ukiharibu mali yako mwenyewe mlalamikaji/ mshitaki ni nani.
Hata zile kesi za jinai ambazo Jamhuri ndio huwa mshitaki bado kunakuwa na shahidi Namba 1(PW1) ambaye ndiye mtendewa(victim). Na huyu kwao ndiye mshitaki. Kwahiyo mshtaki katika tukio lolote la malalamiko lazima awepo.
TATU, ili kosa likamilike lazima uthibitishe NIA OVU. Hii nia ovu unaipata wapi mtu amechomà mali yake mwenyewe.
NNE, kuchoma mali ni kawaida kwa kila mtu. Nyumbani kwako ukikusanya maplastiki, maredio ya zamani, nguo ambazo hupendi na vitu vingine nyie mnajua ukachoma hizo nazo ni mali. Nani kakwambia mali mpaka iwe gari.
Huko vijijini huchoma ardhi katika namna ya kuandaa mashamba. Ni mali inachomwa hiyo.
NNE, Tanzania hatuna sheria inayoelekeza namna ya kuondokana ama kumalizana na vitu ambavyo hupendi tena kuwa navyo. Nyumba huipendi unaweza kubomoa, samani za ndani umezichoka unaweza kuchoma moto, gari limekuchosha unaweza kuchoma ama kuikata vipuri(spare), ni wewe tu na namna yako.
Ni wewe tu kuamua kipi ukifanye mali ya kutunza na kipi ukifanya taka ya kuondokana nayo.
Labda kosa liwe kuwa Moshi uliotokana na uchomaji umedhuru watu, vinginevyo hata mimi nina mpango wa kuchoma ndege yangu binafsi AIRBUS A220 - 300 na nisisikie kelele zeNYU.
Soma: Muimbaji wa injili GodLucky achoma moto gari alilopewa zawadi na mchungaji