Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Ndio imeshakuwa hivyo mkuu cassava, mengi unayoandika ni malalamiko ni kilio chako binafsi ukiwa sehemu umekaa na simu yako ya mkononi, na hayupo wa kukusaidia.

Punguza malalamiko binafsi yakabili maisha kama yanavyotakiwa kukabiliwa. Unakuwa ni wale wale walalamikaji na waliaji wa mitandaoni.

Wakati wewe unaongelea benevolent dictactor wapo wanaoziona fursa nyingi za kibiashara na wanazitumia kikamilifu.

Wewe piga siasa wenzako wanapiga kazi ili wajiingizie kipato.
 
Huyu wakili MWABUKUSI apewe maua yake..
Anafaa kuwa waziri wa sheria au AG
 

Unadhani sina kipato Mkuu! Unasema ni malalamiko yangu binafsi.....Hatua niliyofikia maishani Watanzani wengi ni ndoto! Naona unashindwa hata kuona hao wafanya biashara kufanikiwa kwao bila baraka za CCM.....unataka data katika hili! Unajua Wafanyabishara kinyume cha CCM walifika wapi? Au hauko Tanzania?
 

Steven,

Nisingependa kuitumia kauli hii kwako. maana umesema mimi " ni wale walalamikaji na waliaji mitandaoni" Hapo ndipo unapoona madhara ya CCM, ukitoa hoja kinyume! Wewe ni mlalamikaji na mliaji! Je unapenda na mimi nikuite "CHAWA" ! CCM imejenga mawazo kwa wafuasi wao, kila mtu kinyume na mitazamo ya Chama chao, wewe ni beberu! Hutakii mema taifa hili na upuuzi mwingine!.....all is mob mentality....one line thinking! Wengine wanasema ukiwa CCM lazima ukabidhi akili zako! Ndugu yangu Steven naziona hizo chembe chembe kwako!

Mawazo yenu ndio sahihi! mitazamo yenu ndio sahihi! Raisi wenu ndio yuko sahihi! Mmeshindwa kabisa kuziondoa " Zidumu Fikra za Nyerere" Na kweli zinadumu, angalia tunaogopa kabisa kuangalia Muungano kwa hali halisi ya leo!

Na katika post yako umesema "hayuko wa kunisaidia" In short kwenye maisha yangu sihitaji msaada! Nilifundishwa kuwa indepenent! Hata card ya CCM nadhani nilipata bure nilipoenda JKT.....Na baada ya hapo nilitumia mbali! Niliacha kusoma gazeti la Uhuru na Mzalendo miaka mingi! kuogopa kuwa influence na kuwa brainwashed na CCM!

Mkuu sijasaidiwa na CCM au kufika hapa nilipo!
 
Samia ni tofauti na watangulizi wake, upo uhuru mkubwa wa maoni kulinganisha na wengine.

Angalau tungeutumia uhuru huu kwa kufanya mambo chanya ya kimaendeleo.
 
Ni kama unapiga ngumi ukuta kuwa mbali na CCM, labda uhame nchi ili uwe na amani ya kuishi bila ya chama hiki.
 
Ni kama unapiga ngumi ukuta kuwa mbali na CCM, labda uhame nchi ili uwe na amani ya kuishi bila ya chama hiki.

Mkuu,

Kwangu mimi CCM ni Cult! Kama unavyoona watu wakijiunga na vikundi vya dini ambavyo unashindwa hata kujua ni kwa nini wako huko, ndio kwangu CCM, its a some sort of religious cult! Lazima uwe brainwashed! Nimeona watu wenye akili timamu baada ya kuingia CCM hata reasoning ability waliokuwa nayo kabla ikififia! au kufa kabisa!

Hebu niambie Mwanazuoni kama Kabudi kutoka Chuo kikuu tena upande wa Kitivo cha Sheria kusema katolewa Jalalani! Utasemaje Steven! Kuna tofauti na wale wanaokanyagana na kufa kwa ajili ya mafuta ya Upako!? CCM is a Cult! Hebu niambie Mwakyembe kuyakana maandiko yako mengi alipoingia CCM!Aliyaandika akiwa na akili timamu kabisa! Wako wengi mno watu wa namna hiyo! Hawa ni wasomi, ukiaacha maamuma wengi wanaopewa fulani za kijani na njano kila miaka, hawana zahanati! shule hazina madawati! au waalimu! Utasemaji kama sio nguvu za kudumaza akili toka CCM! +

Je umesahau yule Waziri aliyekua akiyavaa Bendera ya Tanzania katika mavazi yake! Nadhani alisema Magufuli ni Yesu! Kwa mkristo hata Muislamu ni kufuru! Just give me a rational explanation kama sio wameingia kuwa members wa cult fulani!

Mkuu ulisema tumalize huu mdahalo! Hatuweza kukubaliana! Kwangu mimi CCM is a dangerous cult! Na ukiwa Raisi ni zaidi ya Mungu, tuliona hivyo alipokuwepo Magufuli! Aliitumia nafasi yake ya Kiungu mtu ambayo CCM ilimpa! unajua matokeo yake ni nini!

Anyway Steven huwezi kujitambua ukiwa ndani ya CCM, ni ulimwengu mwingine kabisa!
 
Mfumo wa CCM upo tangu miaka hiyo ya sabini, sio chama legelege kama baadhi yetu tunavyodhania.
Mkuu ni kweli, kwenye miaka hiyo (<1970) CCM kilikuwa makini sana, kilikuwa na vyuo vya Siasa pale Kigamboni, Lushoto, Mhiwa n.k. kwa ajili ya kuwafundisha wanachama wake Siasa safi ili kiwe na Viongozi bora. Wakati huo, ili ujiunge na Chama ni sharti usome miezi kadhaa. Hiyo ni CCM ya wakati huo iliyo sheheni Viongozi makini ambao walijua kutenganisha Utendaji wa shughuli za Chama na shughuli za Serikali, kilikuwa Chama kweli kweli kilicho kuwa committed kwa maendeleo ya Watanzania wote "Wafanyakazi na Wakliima"
Leo Chama hakina shule tena, hakina miiko ya uongozi. Wanachama wengi wanapatikana katika mazingira hatarishi, kama siku ya kupiga kura za maoni katika chaguzi wabunge, madiwani au wenyeviti wa mitaa/vijiji; na wakati wa mkopo ya wajasiliamili vijijini. Aidha umri wa Chama kuwepo madarakani kwa kuisimamia Serikali ni mkubwa (miaka 60+) kiasi kwamba kinafanya kazi zake kimazoea.
 
Ni kama unapiga ngumi ukuta kuwa mbali na CCM, labda uhame nchi ili uwe na amani ya kuishi bila ya chama hiki.

Kwa hiyo unakiri kabisa " Huwezi kuishi bila chama hiki (CCM) Inaogopesha sana! Inasikitisha sana! Kweli inanithibitishia kabisa CCM is a Cult! Huwezi kuishi bila yenyewe! Niliwahi kumwambia mtu fulani kuwa CCM is a religious cult! Natamani angekuwa member wa Jamii Forum asome nukuu yako!
 

Chozizwa,

Labda umsaidie ndugu yako, hajui CCM iko kwenye decline! Nimewmwambia kuhusu "Normalcy bias" huko nyuma! Wanadhani mambo ni kama vile jana! Kama wewe ni mwanachama wa CCM msaidie kukirebisha chama kirudi kwenye mstari! Kuna siku Polisi, Tume ya Uchaguzi na hata ma DED watachoka kuibeba! Msaidie mwenzenu!
 
Ni sawa na kuota ndoto nzuri usiku halafu unapoamka asubuhi unakutana na vitu tofauti na vyote ulivyoviona ndotoni.

Itazame Tanzania kwa jicho halisi sio hilo la hisia ulizonazo.
 
Haya maneno tumeyasikia tangu miaka ile Mbowe akiwa mwanaharakati wa gazeti lake mpaka leo hii yanaendelea kusikika kutoka kwa watu mbalimbali.
 
Ni sawa na kuota ndoto nzuri usiku halafu unapoamka asubuhi unakutana na vitu tofauti na vyote ulivyoviona ndotoni.

Itazame Tanzania kwa jicho halisi sio hilo la hisia ulizonazo.

Steven,

Siko njozini! Labda wewe umeshindwa hata kuona Waziri Mbawala kadanganya mchana kweupe! Kama yule aliyedanganya msikitini kuwa Magufuli anachapa kazi! Kumbe kishatangulia mbele ya haki!

Umeshindwa hata kuona Watanzania bara tuko chini ya Kongwa la Wanzanzibari....! Hebu toka usingizini Mkuu! Hiyo Cult itakupeleka pabaya! Ni kama dawa za kulevya!
 
Kwa nini hamfanyi referendum kuondoa zengwe la Muungano?
Referendum hiyo aifanye Nani ? Na kuna Kambi Za majeshi ya Tanganyika kila mtaa wakisaidiwa na Usalama wa taifa mpaka wengine wanavaa rubega Za kimasai. Serikali ya Zanzibar ni ya Tanganyika aliiweka Magufuli kwa mtutu wa bunduki. Na alimweka Kijana wa Mkuranga . Utegemee kuwekwa kura ya maoni ??
 

Kongwa la Mzanzibari gani na ilhali huku Zanzibar mumeweka kambi Za majeshi yenu kila mtaa
 
Wewe unao mlengo wako wa kisiasa na mimi ninao wangu. Mbarawa hajadanganya mahali popote kaeleza sababu za kuingia mkataba na DPW kwamba anao uwezo mkubwa kwa maana ya mtaji, mitambo na uzoefu wa kazi.

Kassim Majaliwa hakudanganya lolote, huwezi kutangaza Rais wako amefariki bila ya bosi wako makamu wa Rais kutangaza kwanza.

Nyerere alitangaza msiba wa Sokoine, alikuwa ni bosi wake. Samia katangaza msiba wa Magufuli, alikuwa ni bosi wa Kassim Majaliwa.

Zipo itifaki za kutangaza msiba wa kitaifa, na mpaka kuzielewa vizuri ni mpaka chama chako kiwe kimeshika madaraka.
 

Kwa hiyo taratibu zinafanya adanganye hata kwenye nyumba ya Ibada! Nimekwambia CCM inaondoa hata hofu ya Mungu! Huyu mwingine anadangamya kuhusu Tenda ambayo ambayo wanaijua wao tu!

Steven, huwa siamini mambo ya ushirikina! Lakini ukiiangalia CCM KWA KINA unaweza kuamini kuna ushirikina unaopumbaza akili za watu!

Huwa nashangaa walioko kwenye fani ya ualimu Tanzania, hivi huwa wanawezeje kufundisha Muundo wa Muungano ambao haungii hata kichwani! Maana Muungano wetu ni kama fumbo la Imani! Haulezeki! Na huwa najiuliza watoto wa Kitanzania wanajua mfumo wetu wa Siasa kweli? Maana hujui tunafuata mfumo wa Kibepari/Ujamaa/Social Democratic......Maana Nyerere alianza na Siasa ya Ujamaa.....na Magufuli akaondoka Fascism!Mungu asingelihurumia taifa hili tulikuwa tumezaa Fashisti mwingine Africa. Mfumo wa siasa ndani ya CCM unamtegemea Raisi! Sasa hivi Samia haijulikani anafanya nini! Hiyo ndio CCM! Lazima ujiondoe akili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…