Wakili CHADEMA athibitisha Mnyika kuitwa Polisi Kinondoni, RPC asema hana taarifa

Naona humu badala ya kujibu mada na kuchangia , vijana tayari wamekula ya ksamulu(Bangi)matusi Tena!
 
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika ameitwa polisi kutoa maelezo kuhusu taarifa ya kutekwa kwa Mshauri wa Chadema Bw. Kibao ambaye baadaye alikutwa ameuawa na mwili wake kutupwa maeneo ya Ununio Jijini Dar es Salaam.

Ni jambo jema Mnyika akatoe maelezo ya kina kuhusu namna alivyopata taarifa hiyo. Aidha ni vema akaambatana na mawakili wa chama ili asije akawekewa maneno mdomoni na pia kupelekwa kusikojulikana!
 
Kama Mimi ni myika na Sheria ikininirusu siendi kwa wauaji
 
Polis nao vichwa boga mbona wanaanza mbele kwenda nyuma washamuita sativa ?
 
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ametakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano, Wakili wa chama hicho amethibitisha...
Yale mambo ya kishenzi ya Magufuli bado yanaendelea!
 
Nashauri asiende peke yake,maana anaweza kupotea tuuu na tusijue aliko,polisi wakiulizwa waseme hawakumwita wao😃😃
 

Vipi ndiyo hao wasiojulikana lakini wanafahamika Polisi ndiyo walioandika barua hiyo kwa katibu mkuu wa CHADEMA kisha yaliyowapata Deusdedith Soka, Mbise na Mlay yamfike John John Mnyika waseme hawajui alipo Katibu Mkuu wa CHADEMA baada ya kupokea wito toka polisi.
 
Huku mtaani sisi tunapambana na hali zetu ila haiwi habari.

Wanasiasa wakiguswa hata na Jani tu wanalia lia na kutaka dunia nzima tulie pamoja nao.

Wanasiasa wabinafsi mno.

Wanasiasa ni kakikundi flani cha matapeli tu wanaojipa mamlaka juu ya wengine.
 
Kama Rais ameshasema ataunda kwanini aende?
 
Nashauri Mnyika Ahojiwe Mbele Ya Vyombo Vya Habari Kwa Uwazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…