Wakili Cleophas Mjema: Uchunguzi wangu umeonyesha kuwa mchakato wa kuharibu uchaguzi serikali za mitaa ulikuwa na hatua zifuatazo

Wakili Cleophas Mjema: Uchunguzi wangu umeonyesha kuwa mchakato wa kuharibu uchaguzi serikali za mitaa ulikuwa na hatua zifuatazo

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,281
Anaandika Wakili Cleophas Mjema,
__________________________________
Uchunguzi wangu umeonyesha kuwa mchakato wa kuharibu uchaguzi serikali za mitaa ulikuwa na hatua zifuatazo:

1. Maafisa wasaidizi wa kata waliagizwa na wakuu wa mikoa na wilaya, kuwashawishi wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa wa upinzani hasa Chadema, waunge mkono juhudi na kujiunga na CCM. Wakifanya hivyo watapewa fedha au nafasi ya kugombea endapo uchaguzi utafanyika. Jitihada hizi hazikuzaa matunda makubwa.

2. Zilichapishwa fomu za aina mbili, feki na halisi. Maafisa waliagizwa watoe fomu feki kwa wagombea wa upinzani na fomu halisi kwa CCM. Feki hazikuwa na nembo ya Halmashauri. Wapinzani walizigundua na kuzikataa. Ndipo amri ikatoka kuwa wote wapewe fomu halisi.

3. Zikaandaliwa fomu feki za kiapo cha maadili ya uchaguzi. Zikagundulika na kukataliwa. Wakurugenzi wakasisitiza kwa watendaji kuwa ni muhimu sana kuwaondoa wapinzani kwa sababu wanakubalika sana.

4. Ahadi ikatolewa kuwa Afisa atakayeokoa kijiji atapata 100,000/= na kitongoji/Mataa ni shiling 50,000/=. Wakuu wa Mikoa na Wilaya pia walikuwa na viwango vyao kwa vijiji na vitongoji watakavyookoa kwa kuengua wapinzani.

5. Wagombea wa CCM waliambiwa warejeshe fomu zao mapema, kisha maafisa wakaagizwa wajifiche. Endapo watabaini uwepo wa uvunjifu wa amani, wapokee fomu zote na kuzipeleka Halmashauri kwa ushauri zaidi.

6. Zilipofika Halmashauri, maafisa wasaidizi walifungiwa mahali pa siri na wakurugenzi waliingia kwa kificho (maana hawahusiki), na kuanza kuelekeza namna ya kuwatafutia sababu wapinzani ili waenguliwe. Kwa mfano, kwenye fomu palipoandikwa WILAYA, wao waliongeza neno "ya" kwa fomu za wagombea wa CCM na fomu za wapinzani zikaonekana hazina neno hilo na kikawa kigezo cha kuondolewa. Hali kadhalika maneno KATA, KIJIJI, n.k yaliongezewa maneno "cha", "wa", nk, wapinzani wakaonekana hawajui kujaza wilaya, kijiji, kata au mkoa.

7. Kwa baadhi ya wagombea wa upinzani waliokataa kuacha fomu zote kwa watendaji, ile waliyokabidhi ilinyofolewa fomu ya katikati na kuipoteza kisha uamuzi ukachukuliwa kuwaengua kuwa fomu zao hazikukamilika.

8. Kuhusu rufaa, leo 6/11/2019 limetoka agizo lenye vipengele vifuatavyo:

Watendaji wajifiche ili wasipokee rufaa. Watakaoshindwa kujificha wapokee lakini watapewa maelekezo na wakurugenzi nini cha kufanya. Kwa kuwa wao ndio waliowaengua wapinzani, hawawezi kuwarudisha kwa sababu utakuwa ni ushahidi kuwa waliwaonea.

Kudhihirisha ukweli kuwa hakuna rufaa itakayobadili matokeo, watendaji wote leo wamepokea fedha zao za kukomboa vijiji na vitongoji. Hawawezi kupokea fedha halafu kijiji kikarudi.

Kwa hiyo kukata rufaa ni kupoteza wakati na Waziri Jaffo anatumika kutuliza tu hasira za wananchi baada ya kuona taharuki iliyopo kwenye jamii!
 
Inamaana wapinzani hawakuwa na nakala za fomu walizorejesha, kwa wale walio fanikiwa kurejesha? Je kuna ushahidi wowote uliokusanywa kuwa wasimamizi wa uchaguzi hawakuwa ofisini kipindi walichotakiwa kuwepo ofisini? Je kuna nakala la hilo agizo unalozungumzia katika kipengele cha 8?

Vithibitisho ni muhimu sana.
 
Teh teh halafu wanasema CCM inakubalika !!! my foooot!!! Labda inakubalika kwa wizi, ufisadi na sina yooote ya uovu.
 
Inamaana wapinzani hawakuwa na nakala za fomu walizorejesha, kwa wale walio fanikiwa kurejesha? Je kuna ushahidi wowote uliokusanywa kuwa wasimamizi wa uchaguzi hawakuwa ofisini kipindi walichotakiwa kuwepo ofisini? Je kuna nakala la hilo agizo unalozungumzia katika kipengele cha 8?

Vithibitisho ni muhimu sana.
Sijui unaishi nchi gani mkuu hadi uhitaji vithibisho kwa haya yaliyotokea
 
Damu pekee ndiyo italeta heshima. Ona kenya
 
Wakili ameeleza ukweli mtupu. Mfano Ni Halmashauri ya Jiji la Mwanza wasimamizi wasaidizi walipopeleka fomu Halmashauri walielekezwa kutenga za CCM na wapinzani kisha waandishi wa Halmashauri wakaelekezwa kutengeneza jedwali ambalo ndani yake wagombea wote wa upinzani waliandikiwa "hakuteiliwa" na wote wa CCM "ameteuliwa."
Lakini kwa bahati, maana Mungu daima humuumbua mtu mwenye nia ovu, mgombea mmoja wa Chadema wa nafasi ya uenyekiti Mtaa wa Igoma Magharibi "A" aliandikiwa kuwa "ameteuliwa" chini yake kukiwa na Wajumbe wote wa CCM, kisha fomu kubandikwa usiku wa kuamkia tarehe 5/11/2019; hata hivyo fomu hiyo ilikuja kuondolewa usiku wa kuamkia tarehe 6/11/2019 na kubandikwa yenye wagombea wote CCM!!!
 
Back
Top Bottom