Wakili Dickson Matata: Uchaguzi unatakiwa uwe huru na wa haki

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Imeelezwa kuwa kushiriki katika uchaguzi ambao hauko huru na wa haki ni kukiuka misingi ya demokrasia na kuhalalisha dosari za mfumo wa uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Wakili Msomi, Dickson Matata wakati akizungumzia uamuzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025.

Akizungumza katika kipindi cha Jambo Asubuhi, Wakili Matata amesema uchaguzi unapaswa kuwa huru na wa haki ili kutoa nafasi sawa kwa Vyama vya siasa na Wananchi kuchagua viongozi wao kwa uwazi na uaminifu.

Amesema iwapo uchaguzi hautazingatia misingi hiyo ya kidemokrasia, kushiriki katika mchakato huo kunakuwa sawa na kuhalalisha kasoro zilizopo katika mfumo wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa Matata, ndiyo sababu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliweka msimamo wa kutoshiriki uchaguzi huo hadi pale kutakapopatikana Katiba Mpya na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, hatua ambazo anaeleza zitasaidia kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki na unaoaminika kwa pande zote.

Pia soma: GE2025 - Wakili Dickson Matata: Unaingiaje kwenye uchaguzi ambao Rais ambaye ni Mgombea ndiye anayeteuwa Mwenyekiti, Makamu na Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi
 
Kushiriki kwenye uchaguzi usio Huru na Haki ni sawa na kushiriki kwenye kutenda Uhalifu
 
My friends, ladies and gentleman,
sote ni mashahidi kwamba chaguzi zote Tanzania tangu tupate uhuru na kuingia kwenye mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, hufanyika kwa uwazi, uhuru na haki.

changamoto na dosari za kawaidi kama vile waliokataliwa na wananchi kwa kura kuleta fujo kwenye vituo vya kupigia kura ni za kawaida na hazina athari sana hata kubadili ukweli huo kwa mujibu wa sheria.

Serikali sikivu ya CCM itaendelea kuboresha mazingira bora na yenye usawa zaidi kwa vyama vya siasa na wananchi ile wale wote wenye sifa za kisheria, kushiriki vyema kwenye mchakato huo wa kidemokrasia nchini.

umoja, amani na mshikamano miongoni mwa waTanzania vitalindwa kwa nguvu na gharama yoyote ile.
 
Jinga wewe
 
Back
Top Bottom