Wakili Haji Nanduli: Kila Lita ya Petrol na Dizeli kuna Tsh. 50 inayoenda Mfuko wa Taifa wa Maji

Wakili Haji Nanduli: Kila Lita ya Petrol na Dizeli kuna Tsh. 50 inayoenda Mfuko wa Taifa wa Maji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji, Wakili Haji Nanduli ameeleza kuwa kwenye kila lita moja ya mafuta ya Petrol na Dizel ukatwa Tsh. 50 kama tozo kwa ajili kupelekwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Maji ili kuwezesha utekelezaji wa mradi ya maji nchini.

Ameongeza kuwa ili kuwezesha upatikanaji wa Maji, wamekuwa wakitoa pesa kwa utaratibu wa ruzuku kuwezesha miradi ya maji mbalimbali inayotekelezwa hususani maeneo ya vijijini, lakini pia ameeleza kwamba wamekuwa wakitoa mikopo kuwezesha miradi ya maji kutekelezwa kwenye baadhi ya maeneo.

Pia amasema kwamba karibia kila mwaka kiasi cha fedha kisizopungu 60% kutoka ya pesa zote ambazo utolewa na Mfuko huo uelekezwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ili kutekeleza miradi ya maji vijijini.
 
Back
Top Bottom