Wakili Kambole: Hakuna kosa kisheria mtu kupiga picha akiwa na fedha zake

Wakili Kambole: Hakuna kosa kisheria mtu kupiga picha akiwa na fedha zake

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
1720691732991.png

Wakili wa kujitegemea Jebra Kambole amesema kuwa, hakuna kosa kisheria kwa mtu pale anapoamua kupiga picha akiwa na fedha zake.

Wakili Kambole amesema hayo Julai 10, 2024 alipokuwa akihojiwa na kituo cha redio cha ambapo amesisitiza kuwa, endapo mtu akikamatwa kwa kosa hilo ana uhalali na uwezo wa kumchukulia hatua za kisheria aliyemkamata.

"Kupiga picha na fedha haiwezi kuwa kosa la jinai, mtu akikamatwa kwa hilo kosa (la kupiga picha na fedha zake) anaweza akachukua hatua za kisheria" alisema Wakili Kambole na kuongeza "Hakuna sheria inayokataza kitu cha namna hiyo, sheria inakataza kuharibu fedha kama vile kuichana na si kupiga picha. Hakuna kosa kwa mtu anayepiga picha kuonesha fedha zake mwenyewe".

Itakumbukwa hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda alikaririwa na vyombo vya habari mbalimbali nchini aklitaka jeshi la polisi wilayani humo kuwakamata watu wote ndani ya wilaya hiyo ambao wanachapisha maudhui (post) za kujinasibu kwamba wana hela kupitia mitandao ya kijamii.

Kama habari hiyo ilikupita soma hapa: DC Temeke: Mtu akipiga Picha na hela akamatwe
 
Back
Top Bottom