PostGE2025 Wakili Madeleka: Katiba mpya itajibu mahitaji ya sasa ya Watanzania

PostGE2025 Wakili Madeleka: Katiba mpya itajibu mahitaji ya sasa ya Watanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Wakili Peter Madeleka, akiwa kwenye mjadala wa Jambo TV ulioangazia matukio yaliyotokea kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu, amesema tathmini yake inaonesha kwamba watu wengi wanaamini kuwa Katiba Mpya ndio inaweza kuwa chachu ya kupatikana kwa majibu ya changamoto zinazotokea nchini kwa sasa

Katika maelezo yake, Wakili Madeleka amesema Katiba inayotumika sasa Tanzania ya mwaka 1977 haina majibu ya moja kwa moja ya maswali na hoja za kizazi cha sasa, na kutokana na ukweli kwamba Katiba hiyo iliundwa wakati nchi ikiwa kwenye mfumo wa chama kimoja cha siasa
 
Bado na yeye anatakiwa kunyoosha maelezo! Aseme tu ukweli wananchi wanataka ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba irejeshwe mezani! Ile Rasimu iligusa karibia maeneo yote muhimu yaliyo lalamikiwa na wananchi.

Kuanzia kwenye kupunguza mamlaka makubwa ya Rais kwenye maamuzi na uteuzi, suala la muungano, kupunguzwa kwa matumizi ya serikali kwa kuviondoa vyeo vya kisiasa na kupunguza ukubwa wa bunge, nk.

CCM wakiachwa peke yao kwenye ishu ya Katiba mpya, wanaweza kubadilisha jina tu kama walivyofanya kwenye tume ya uchaguzi kwa kuongeza neno "huru", huku hiyo tume ikiwa ni ile ile ya zamani.
 
Angepewa ubunge asingesema haya, ni sawa na kiongozi wake Zitto.
 
Yeye si alisema hakuna wa kumshinda Jimbo la kivule labda sir 100
 
Kuanza mchakato wa kuandika katiba mpya ni kupoteza rasilimali nyingi bure. Katika mazingira yetu ta kisiasa na kiutawala, katiba yoyote itakayoandikwa itabeba zaidi tamaa za wanasiasa kuliko matakwa ya wananchi. Tuboreshe tu katiba yetu iliyopo, ili iendane na wakati.
 
Back
Top Bottom