Wakili Madeleka: Paul Chacha ajue kwamba amefanya kosa aombe radhi kwa Sofia

Wakili Madeleka: Paul Chacha ajue kwamba amefanya kosa aombe radhi kwa Sofia

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wakili wa kujitegemea, Peter Madeleka, amemtaka aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, kuomba radhi kwa mwanamke aliyetambulika kwa jina la Sofia kufuatia kitendo chake cha kuweka hadharani jumbe na mazungumzo yao ya faragha.

Akizungumza kuhusu sakata hilo, Wakili Madeleka ameeleza kuwa iwapo Paul Chacha alikuwa hafahamu kuwa kusoma ujumbe wa faragha hadharani ni kosa, anapaswa kutambua sasa kuwa amefanya kosa la kisheria. Ametaja kuwa mawasiliano hayo yalihusu watu wawili pekee na yalipaswa kubaki kuwa siri.

Amefafanua kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalinda haki ya faragha ya kila mwananchi, ikijumuisha faragha ya mawasiliano, msingi uliosababisha pia kutungwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi za Watu.

"Jambo linalofanyika faraghani ni la binafsi, na mtu akilileta hadharani linaweza kutafsiriwa kama udhalilishaji. Ni kosa kudhani kuwa taarifa za binafsi walizopeana kwa faragha zinaweza kutumika kama mtaji wa kisiasa," amesema Madeleka.

Soma pia

 
Ingekuwa nchi za ulaya na amerika angepandishwa kizimbani kumlipa fidia huyo mwanamke na kulazimika kujiuzulu
 
Back
Top Bottom