Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), William Maduhu akihojiwa na Wasafi FM leo Mei 20, 2026, amezungumzia mamlaka ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu utoaji wa faini kwa vyama vya siasa, akibainisha kuwa Msajili anatumia kifungu cha 19 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ambacho hakimpi mamlaka ya kuwa chombo cha udhibiti wa kutoa adhabu. Amesema kuwa nchini kuna mamlaka za udhibiti kama Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambazo kwa mujibu wa sheria zinaweza kutoa faini au kuendesha mashauri yenye sura ya kimahakama, tofauti na Msajili ambaye hana mamlaka hayo.
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa sheria, utoaji wa faini au adhabu za kifungo ni jukumu la mahakama pekee, hivyo hatua ya Msajili kutangaza adhabu za faini kwa vyama vya siasa ni kujipa mamlaka ambayo hana. Ameongeza kuwa Msajili hana sifa ya kuwa mamlaka ya udhibiti (regulatory authority), na hivyo hana mandate ya kutoa adhabu hizo kwa vyama vya siasa.
Soma: Nyahoza: Barua yetu kwa CHADEMA inasema kusimamisha chama kwa muda, sio kufuta
Aidha, Wakili Maduhu ametoa wito kwa mamlaka za nchi kuwa na ustahimilivu katika masuala ya kisiasa, akisisitiza kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi vya siasa na kauli za majukwaani zinapaswa kujibiwa kisiasa na si kwa hatua za kiusalama au kisheria. Amesema ni vyema mijadala ya kisiasa ibaki majukwaani badala ya kuingizwa katika vyombo vya usalama au mahakama, ili kudumisha uhuru wa maoni na ustahimilivu wa kisiasa nchini.