Kiongozii FMSE, Heshima mbele Mkuu;
Ni vema tukajifunza uvumilivu hasa pale watu wanapoongea facts badala ya wewe kuwa dissapointed pale watu wanapohoji mambo ya kimsingi au wanataka kusema ya kweli.
Uliongea mengi sana kuwa wewe uko close naye na ukajenga mazingira halisi kuwa uko karibu sana na familia ile. Ukajibu hoja nyingi sana lakini ulipoulizwa katika hayo masuala mawili ukashindwa kujibu na kudai hutaongelea hilo. Kama hutaki kuwa dissapointed tuletee majibu ya mswali hayo kuwa alikwepaje JKT na aliingiaje UDSM bila kuwa na cheti cha JKT. I will be OK.
Kama kuna kiongozi yeyote unayemjua hata humu JF ambaye hapendi kufuata utaratibu na unamjua, jibu ni kumtaja na kumsaidia wapi alikosea na wala si kuwa na wasiwasi kuwa tutaibua mengi. Tumechoka sasa na haya mambo ambayo ndiyo yametufikisdha hapa tulipo miaka 47 baada ya uhuru ingawa tuna rasilimali zote za kuleta maendeleo. Inatia uchungu sana.
FMSE mimi ni moja kati ya watu wanaokuheshimu sana hasa kwa kuleta datas. Na nakuhakikishia kuwa post zako zote nimekuwa nikizisoma. Hunijui ni nani na wala mimi sikujui ni nani. Mhusika pia ni namfahamu kiasi japo inaweza kuwa si karibu sana kama wewe. Lakini inapokuja suala la ukweli na maslahi ya taifa, wengine sasa tumechoka na tumeamua kujitoa mhanga kwa ajili ya taifa hilia come what may. Just wait and see. Call a spade spade. Black balck and white white.
Katika uongozi historia na tabia ya mtu has something to do with the future. Hasa kama mhusika hataki kujisahihisha. Its is the history which shapes the future. Nina imani wahusika walikuwa wanajua ni nini kinaendelea katika suala la Deep Green hasa ukiangalia facts zote ambazo Dr. Slaa alizitoa bungeni.
Nakusihi na kukuomba kuwa, wakati huu ni wa kusimama pamoja na kuwa wakweli bila kujali kama mhusika mna uhusiano naye kivipi. Ni kwa kufanya hivyo mimi, wewe na wote tutalirekebisha taifa. Dawa ya jipu ni kulitumbua na kutoa usaha. Japo litauma lakini utapona. Sisi ni watu wazima, kubali kiungwana kuwa yatupasa tuwajibike.