Wakili Mediam Mwale adaiwa kukutwa na TZS 18 bilioni haramu

Wakili Mediam Mwale adaiwa kukutwa na TZS 18 bilioni haramu

Naomba kujuwa wakili Mwale . Anakabiliwa na Kesi gani iliyomfanya kukaa mahabusu miaka 7 mpaka sahiv.
 
Nilisikia alikuwa anafua pesa hadi zinatakata..so kosa la kutskatisha ndilo linalomkabili...sina uhakika sana wajuvi waje
 
Ngoja wajuvi wa mambo waje. Ila kiukweli siku hizi mikoa ya Arusha na Moshi ujambazi umepungua sana,sana tu. Na huyu ndo alikuwa wakili mkubwa wa wajanja wa mikoa hii. Nahisi ipo namna wamemtengenezea zengwe yeye pamoja na network yake.
 
Kesi ya Kutakatisha Fedha, Na Hayupo Mahabusu, Yupo Kisongo Gerezani, Nenda Utamkuta
 
lema alikuwa anamtetea sana, sijui ni ule msemo wa waswahili wa pemba hujuana kwa vilemba..
 
Nyaga si alikufa kifo cha kutatanisha vile? Na alizikwa wap vile? Kuua nini ile?
 
Wanasheria wengi wao esp Huko Arusha nadhani hiizi deal za viwanja wana husika sana, TAKUKURU iwachunguze na Halimashauri za Miji zitupe details za ukweli wakina nani wana Hold maeneo makubwa na esp kwa Wanasheria Tu ndio Mtajua wanasheria wetu kwa kiasi gani wanatuhujumu nchi yetu.


Hizi deal huwa zina mikono mirefu behind them
 
WAKILI maarufu nchini, Mediam Mwale aliyekuwa akishikiliwa na polisi tangu Agosti 2, mwaka huu, jana alifikishwa mahakamani akidaiwa kukutwa na fedha haramu zaidi ya Sh18 bilioni.

Mwale alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Arusha, Charles Magesa ambaye hata hivyo, alikataa kupokea hati ya mashtaka baada ya kugundua makosa ya kisheria.

Wakili huyo anakabiliwa na mashtaka 13 ambayo Hakimu Magesa alisema shtaka la tatu hadi 13 hayaonyeshi ushiriki wa moja kwa moja iwapo mshtakiwa alilipwa au alipata fedha kupitia kampuni, taasisi au shirika kutokana na hati hiyo kutofafanua jambo hilo.

Mashtaka dhidi ya wakili huyo yalisomwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Velitasi Mlau aliyedai kuwa hati hiyo imekamilika na inajitosheleza ndiyo maana imewasilishwa mbele ya mahakama.

Wakili wa utetezi, Loomu Ojare alipinga hoja ya wakili huyo wa Serikali akitaka upande wa mashtaka kujipanga upya na kueleza tuhuma zinazomkabili mteja wake, idadi yake na aina ya tukio badala ya kuwasilisha mashtaka ya jumla yasiyojitosheleza kisheria.

Hakimu Magesa alikubaliana na kosa la kwanza hadi la tatu na aliahirisha kesi hiyo kwa kuuagiza upande wa mashtaka kurekebisha hati hiyo na kuirejesha mahakamani ikionyesha kwa usahihi kampuni iliyompa fedha wakili huyo.

Kutokana na uamuzi huo, Wakili Mwale alirejeshwa mikononi mwa jeshi la polisi wakati upande wa mashtaka wakitekeleza amri ya kurekebisha hati ya mashtaka kabla ya kuirejesha upya mahakamani.


Chanzo: Mwananchi
Hii iliishaje??
 
Back
Top Bottom