Wakili Msomi, Naibu Spika, Mhadhiri Mwandamizi na Daktari wa Falsafa wa Sheria, Tulia Ackson awa tishio kwa Spika Job Ndugai

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Katika kuunda Timu yake ya kuhakikisha anazidi kubaki madarakani - Mh. Spika, Ndugu Job Ndugai amegundua tishio au threat (kwa kimombo) kubwa kwake ni Naibu wake.

Huyu bwana mambo mengi amekuwa akiyafanya kwa kutumia vitisho vitisho tu akiachana kabisa na ule utaratibu wa kidemokrasia wa Mtangulizi wake Marehemu, Msomi Wakili, Samweli Sitta.

Huyu anataka kuwaonesha watu kuwa wanasheria si lolote na si chochote. Kwa kuweka msisitizo huo ameanza kuwashambulia eti watu wanaotambulishwa kwa majina ya fani zao waache mara moja.

Hii ina maana hataki Naibu wake atangulize utambulisho wa fani au umahiri wake kwa sababu wakigombea pamoja USpika ni lazima hizo sifa za fani na umahiri zitampunguzia credit.

Waliokuwa karibu na Naibu Spika jana baada ya maneno ya Bosi wake wanadai alishangaa sana na lugha ya machoni alionekana kutoafiki aliyokuwa akiyaongea Bosi wake.

Siku hizi za karibuni Job Ndugai amekuwa akitumia sana ubabe kuongoza bungeni na kutamani kuongoza hata mihimili mingine ili aonekana ana nguvu kubwa ya kimaamuzi hapa nchini kwani baada ya kujihisi hataweza kugombea URais 2025 amepania agombee tena huo USpika.

Wabunge wengi wanamchora tu na kujifanya wanamuunga mkono lakini 2025 ni lazima aliwe kichwa na asipokuwa makini akajaribu kugombea basi changamoto ya kisaikolojia itamkumba na kumsababishia shinikizo la damu na kitachofuata mimi sijui.

Ninamshauri amwandae Naibu wake kushika 2025, hiyo ndiyo salama yake.
 
Kipindi cha miaka kuelekea saba/name iliyopita nawalaumu Sana mzee wa bakora,naibu wake, na aliyependwa zaidi,kwakutiharibia taifa letu. Hivyo sitamani watu hawa wawe hata na nafasi ya ujumbe wa nyumba kumi, sababu no nyingi, sheria zote kandamizi na mbaya ni zawakati huo, achilia mbali uonevu, ubabe, unyanyasaji na ubambikiaji.
 
Hivi spika anaweza kuwa kwenye nafasi yake kwa muda wa miaka mingap?
 
Huyo Naibu wake nae mbona ni mtu mwenye tabia kama zake? Ubabe na kujisikia ndio style zao za kuliongoza Bunge.

Tena afadhali ya Spika yeye ana base and background ya siasa kuanzia jimboni pale Kongwa. Lakini dunia nzima inajua Naibu Spika aliivyoingia Bungeni kwa mbeleko ya waziwazi ya Mwendazake na kisha zile sarakasi za kitoto kabisa za pale Mbeya mjini

Wapo watu wanaofaa kwa nafasi zote hizo mbili yaani uSpika na naibu wake lakini sio hao wa sasa. Acha tu waparurane
 
Ngoja kwanza atafute nyingine za kwenda kutibiwa india.....
 
Nimependa hapo ulipomalizia "acha waparurane"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…