wakili msomi Silas Isangi ambae ndie rais wa RT. Aongeze juhudi

wakili msomi Silas Isangi ambae ndie rais wa RT. Aongeze juhudi

Joined
Feb 25, 2021
Posts
11
Reaction score
9
Leo nimeona nimstue kidogo wakili msomi Silas Isangi ambae ndie rais wa RT.

Kiukweli tangu achaguliwe kua rais wa RT tumekua na matumaini mapya juu ya Riadha ya Tanzania. Lakini cha kusikitisha, tangu Silas achaguliwe, zaid ya kua mdandiaji wa mbio zinazoandaliwa na vyama vya mikoa mbalimbali (hasa Arusha) hakuna kingine anachoonekana kua anafanya kwa maendeleo ya Riadha nchini.

Badala yale Silas amemuachia kila kitu kihiyo John Bayo ambae mpaka sasa uteuzi wake ni kaa la moto. Silas amekua mtu mwepesi kuliko ilivyotarajiwa. Licha ya kwamba huyu mtu ni mwanasheria mbobevu, ameruhusu kuwekwa kwapani na bwana Bayo kiasi inaleta mashaka kama na yeye yuko kwenye payroll ya Bayo kama walivyo kina Msitha ama kuna nini cha ziada.

Silas mpaka sasa hakuna chochote alichofanya na badala yake kumuacha Bayo kua ndie katibu wa RT, Mkurugenz wa ufundi wa RT, kocha wa RT nk. Huyu Bayo mkumbuke ndie yule ambae hata cheti cha form four hana achilia mbali Diploma, elimu ambayo ndio inatakiwa kikatiba kwa mtu anaeshika nafasi ya Makamu wa Rais RT. Bayo sasa na kazi za kuvamia mbio zote zinazoandaliwa na watanzania na kupoka majukumu ya vyama vya riadha vya mikoa lengo ikiwa ni kupiga deals, pia bayo kwa miaka mingi amekua wakala wa wachezaji wa nje na inapokuja swala la mialiko ya wachezaji wa nje yuko tayar kugimbana na yeyote mradi wachezaji ambao yeye ndio wakala wao wa hapa nchini waje na kushiriki.

Mfani rahisi wa bwana bayo ni mashindano ya Tulia yaliofanyika hivi karibuni mjini Mbeya ambapo alifikia hatua ya kuforge sahihi ya mama Ombeni Zavala ili kuwatumia mwaliko wana riadha wa Kenya kinyume na taratibu za mialiko zilizowekwa na BMT. Mama zavala mwenyewe alipoulizwa kama ndie alieandika barua alikana na kusema hakuwah kupata maelekezo hayo na kusema sahihi yake iko ya kielektronic kwenye kompyuta za RT na huenda alieforge alizipata huko.

Bwana Bayo hakumaliza form four baada ya kufukuzwa kwa kosa la kumtia mimba mwanafunzi. Na amekuja RT kupiga na si vinginevyo. Pia mkumbuke huyu Bayo ni mmoja kati ya wale madiwani wa Arusha waliokua chadema na kukisaliti chama chao kwa mlungula katika uchaguz wa Meya wa Jiji la Arusha. Magumashi ndio mfumo wa bwana Bayo kwa miaka mingi.

Malalamiko dhidi ya Bayo yako BMT na mwanaharakati Whilhem Gidabuday mara kadhaa ameeleza hadharani kupitia vyombo vya habar juu ya bwana Bayo kukosa sifa za uongozi lakini viongozi wa wizara na BMT wamekua na kigugumumizi kuchukua hatua, na kupeleke mpaka sasa RT kutokua na Dira inayoeleweka, kwan Bayo hana weledi wala Elimu, wakati huo huo Silas hana muda wa kushughulikia mambo ya RT.

Bwana Silas, tunakupa muda hwbu simamia katiba ya RT, kumbuka mtaka alienguliwa kwa kosa la kushindwa kusimamia katiba basi na ww usirudie hilo kosa. Itisha vyeti vya wote waliochaguliwa na ujiridhishe kama wana sifa za kikatiba kushika nafasi walizonazo. Huu ndio mtihani wako wa kwanza. Tunaahidi, kukaa kimya hakutafanya hili jambo liishe.

Wakati wa kutenda ni sasa.
 
Back
Top Bottom