TANZIA Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

RIP Prof. Jwani Mwaikusa.

Tunakubali kifo kitamkuta kila mmoja wetu, ila Serikali ina haki ya kikatiba kuwa linda raia wake.
Kwa serikali yetu jambo hili ni kinyume chake. Polisi ndo wanaolinda majambazi!!! Eti siku hizi wanasema watu walinde mitaa (polisi jamii)

Poleni wafiwa, Mungu awatie nguvu na imani katika wakati huu mgumu. Tulimpenda lakini yeye kampenda zaidi. AMEN.
 
Tatizo letu kubwa ni kwamba crimes nyingi sana za homicide zimekuwa zikichukuliwa kwa urahisi rahisi tu kama ajari za moto, magari, au mauwaji ya ujambazi na kwa kadri ninanvyojua mimi polisi wetu ama kwa uzembe au makusudi ama kwa kutokuwa makini na kazi zao wamekuwa wakihalisha na kufunga mafaili ya homicide kama ajari au ujambazi wa kawaida.

Ninadhani ni wakati muafaka tukaanza kuwa na desturi ya kuchunguza kwa undani na kuweza kufanya hivyo inabidi ajira za jeshi la polisi au kitengo cha homicide zikaangaliwa upya ili watu wanaoajiliwa wawe watu makini na siyo drop outs au watu waliofeli mitihani yao kwenye ambao wanatafuta upolisi kama last resort katika kutafuta riziki.
 


Not acceptable pls. We deserve better than this!
 

Sasa kwa mambo haya wameitaji majambazi wakati hawajaiba chochote? they should say black and white ni MAUAJI.
 

Another actors; sijui itakuwa season ya ngapi?
 
Poleni wafiwa. Kama alitetea hoja ya mgombea binafsi, nina wasi wasi kuna mkno wa wale wale, wabongo tunatawaliwa na jinamizi ambalo silielewi, nguvu za giza..for how long will this last. Kutawaliwa kimafia ni risk kubwa jamani! Nadhani mwisho wetu ni mbaya!
 
Kama wamempiga head shot kwakweli itakuwa assassination.
 
Mungu awatie nguvu na imani katika wakati huu mgumu. Tulimpenda lakini yeye kampenda zaidi. AMEN.
"Kampenda zaidi" ndio amuache achinjwe hivyo na mwanae? Yani sisi tunaompenda kidogo tunamwonea hurumu huyu Mungu anaempenda zaidi hana huruma, Mungu gani? "Awatie nguvu katika wakati mgumu" wakati mguu saa ngapi tena, wakati mgumu ni pale wakikatwa roho, ndio pale Mungu angetaka angeibuka akawatia nguvu marehemu, hakutokea, bado tunamsubiri? Hata polisi walikuja baadae.
 
Poleni wafiwa na Watanzania wote kwa kumpoteza mtu muhimu katika familia yake na taifa kwa ujumla. Ni wazi haya ni mauaji na wala sio ujambazi, lakini wahusika lazima waelewe kwamba ipo siku watalipa wao na vizazi vyao.

R.I.P Prof Mwaikusa, tutakukumbuka.
 
Ndo keshakufa hivyo. Hakuna cha kufanya isipokuwa hao waliomuua hukumu yao ni hapa hapa duniani siku sio nyingi. Polisi inapaswa kubeba lawama zote. RIP Prof.
 
Kama namsikia IGP Akiongea na watu wa tasnia ya habari "Nimawaeten blah blah ....then nitaunda tume ya watu 7 kuchunguza mauaji haya blah blah..."

Kila siku huwa tunafanya kazi kwa stahili za kizimamoto.
 
Kutoka Michuzi Blog:


BREKING NYUUUUZZZZZ: PROFESA MWAIKUSA AUWAWA JIJINI DAR
Marehemu Profesa
Jwani Timothy Mwaikusa


Habari zinasema Wakili na Mwanasheria nguli na Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof. Jwani Timothy Mwaikusa amefariki dunia baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati akirejea nyumbani kwake maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam.

Prof. Mwaikusa pia alifanya kazi katika mahakama ya kimataifa ya I.C.T.R Arusha na alikua rafiki wa mahakama ambaye alitetea vizuri hoja alizowasilisha kuhusu mgombea binafsi.

Kwa wale waliosoma literature A- Level kama mimi, Prof. Mwaikusa pia alikua mwandishi mzuri wa poems ambazo wengi wetu tulizijibia mitihani.
Pamoja nae pia ameuwawa mwanae aliyekua akitoka nje kumfungulia geti, na mtu baki aliyekua akipita njia.

Kwa jicho la kawaida tu, haya yatakua mauaji ya kisasi au ya kumnyamazisha kuhusu jambo fulani kwakua habari za awali zinasema wauwaji hao hawakuiba kitu chochote

Na Mdau Nkundwe Mwakilema

NILIYOYAFAHAMU:
Career:
* Professor of Law, Faculty of Law, University of Dar es Salaam 1999
* Mkono & Co Advocates since 1998
* Advocate, High Court of Tanzania since 1988
* Managing Editor of the Tanzania Law Reports.
Qualifications:
* Ph.D., School of Oriental & African Studies, University of London, UK, 1995
* LL.M, University of Birmingham, UK, 1985
* LL.B (Hons), University of Dar es Salaam, Tanzania, 1981.
 

Mungu ailaze roho yake pema peponi...well, kwa bahati mbaya watu makini ndio wanatangulizwa kwanza mbele ya haki ili mabazazi waendelee kupeta. Hao majambazi sijui wanajua ni kwa kiasi gani Taifa limepoteza mtu makini? Na naendelea tena kujiuliza, inakuwaje wavamie nyumba yake usiku? Alikuwa na benki nyumbani kwake? Ukweli unatabia ya kujitenga na uongo...ipo siku ukweli utawekwa bayana
 





Nadhani unaamanisha wakati alipokuwa anakaribia kumtaja mgombea mwenza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…