TANZIA Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

TANZIA Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

Mkuu, with all due respect naomba usianze mambo yako ya kuingiza kila kitu kwenye siaza tafadhali... IT IS TOO EARLY!!!
Mkuu De Novo kwani kuna nini kati yako na Mwanakijiji? Unakisilani naye? unaugomvi naye? Unashindwa kuona ameanza na neno inawezekana? hilo neno laonyesha hana hakika, iweje sasa unamhukumu kwa asilimia 100% Nimesoma post zilizotangulia kuna waliotoa hisia zao bila kutumia neno inawezekana na wala hujawashukia kama ulivyofanya kwa Mwanakijiji. Tueleza basi kama mlingombana naye, vinginevyo tunashindwa kukuelewa una ajenda gani.

RIP Prof. Mwaikusa
 
Huu ni ujambazi wa kawaida tu nadhani. Tuone polisi wetu watalifanyiaje kazi hili. Lile la yule wakili rafiki ya Mkapa walilifanyia kazi kwa spidi ya ajabu.
Hakuna mwenye uhakika kwa sasa, yawezekana siyo majambazi, ila kwa sasa tuseme ni watu wasiojulikana wamewaua Prof. Mwaikusa na Mwanawe.
 
Nadhani unaamanisha wakati alipokuwa anakaribia kumtaja mgombea mwenza.
Ni wakati wa kurudisha madaraka ya rais na serikali kwa wananchi ili Watanzania wawe salama zaidi. Kwa sasa madaraka ya rais na serikali yapo kwa rais badala ya wananchi. Watanzania turudishe madaraka mikononi mwa wananchi kutoka kwa rais na serikali.
 
Mkuu sifahamu hata muuaji mmoja, lakini naweza kusema hakuna mnyarwanda anayeweza kuja kumuua huyo jamaa kwa kuwa judge tu wa ile mahakama. Tusiumize vichwa kwa sasa, he is already dead, in weeks and months ahead tutajua muuaji ni nani, for sure hata kamatwa and life will go on. Hii ndio haki Tanzanian style.
Kama haumfahamu muuaji kwa asilimia 100% unawezaje kusema fulani hahusiki?
 
mmh nahisi mbinu chafu hapa,hasa kwamba prof alikua jaji I.C.T.R.hii kufungua milango ya E.A.C.nayo watu wanaweza kuingia wakammaliza kisha wakarudi kwao kimya.
 
R.I.P Profesa Mwaikusa, mwanao na huyo mwengine asiye na jina. Mwenyezi Mungu zipe nguvu familia zenu.

Amandla....
 
Kwa sasa hivi inafahamika kuwa ni majambazi. Nadhani uchunguzi wa kina baadaye ndio utakaoonyesha iwapo kuna mkono mwingine
R.I.P Prof
Hapana mpita njia hatuwezi kusema ni majambazi wakati hatujui muuaji kwasababu muuaji siyo lazima awe jambazi. Ni sahihi tukisema ni wauaji wasiojulikana.
 
''When the person you love becomes a memory, the memory becomes a treasure''
 
Sijui ni kumbukumbu zangu au ndio uzee wenyewe.... kuna wakili mmoja aliuawa miaka michache iliyopita kwa staili hiyo hiyo, halafu sijui ni mwaka jana ule ambapo msomi mwingine toka UDSM aliuawa kwa staili ile ile.. (jina limenitoka kidogo) na sasa Mwaikusa. Aidha hawa "majambazi" wanapenda sana wasomi tena mawakili.. au
 
Nasikia siasa zimetawala kwenye mazingira yote ya kifo chake!

Nimejaribu kutafakari hisia za baadhi ya wachangiaji ... kujaribu kuunganisha haya mauaji na lile suala la mgombea binafsi lakini nimeshindwa kupata any dot to join..
Yeye alikuwa ni mshauri/rafiki wa mahakama na alitoa ushauri wake kulingana na alivyoliona shauri. Mahakama haikutilia/ilitilia maanani ushauri wake na kesi ikaamuliwa vile ilivyoamuliwa. Je ukiamua 'kumwondoa' sasa baada ya kesi kwisha kutakuwa na impact yeyote kwenye ile hukumu iliyokwisha somwa? Jibu langu ni hapana. Hivyo, mimi nafikiri sababu za mauaji zitakuwa ni nyingine zaidi ya hii ambayo baadhi ya wachangiaji wameihisi.
Ujambazi?
Kisasi?
Bila info zaidi ni vigumu kuelewa.
RIP Professor wetu Mwaikusa
 
Sijui ni kumbukumbu zangu au ndio uzee wenyewe.... kuna wakili mmoja aliuawa miaka michache iliyopita kwa staili hiyo hiyo, halafu sijui ni mwaka jana ule ambapo msomi mwingine toka UDSM aliuawa kwa staili ile ile.. (jina limenitoka kidogo) na sasa Mwaikusa. Aidha hawa "majambazi" wanapenda sana wasomi tena mawakili.. au

Mi ndiyo nimezeeka zaidi kwani hata sikumbuki matukio unayorejea, kweli uzee unatujia mapema sana!
 
Mi ndiyo nimezeeka zaidi kwani hata sikumbuki matukio unayorejea, kweli uzee unatujia mapema sana!

tunasahau kirahisi tu.. ndugu yangu.. si unaona hata majina mia yamenitoka.. yule wakili aliuawa sijui maeneo ya Msasani kule na yeye vile vile akiingia nyumbani, na huyu mwingine sijui maeneo ya Ubungo huko karibu na baa yake or something like that..
 
Akiwa anakaribia kutaja mgombea binafsi naomba nimnukuu RAIS,DK KIKWETE

Mimi napenda niwaonye kabisa yoyote atakaeshabikia ama kutaka kufanya kitu kitakachotutenganisha
nawaambia kweli hii serikali si sehemu ya kutafuta umaarufu,,nasema hili nikimaanisha nawambia ili mtu asishangae ..kuna walioanza chokochoko tuliwashugulikia na wengine (

tumewasahau)

kabisa

Mwenye akili utajua ana maana Gani!!!nawaambia ukweli tutakushugulikia mpaka mwisho..mi nawaambia msidanganyike bwana kitu kikija kwangu nikisema no ni no hata iweje..utahangaika kwa haki za binadamu ,,mahakama kuu na vyombo vingine vya sheria nikisema no itaishia no

DK KIKWETE TUELEZE PROF WETU ALIPO...HILI JAMBO WANA JF SI LA KUCCHUKULIA MZAHA HATA KIDOGO..ATUITAJI KUISHI NA SERIKALI YA WAUWAJI..UTAMUUA KILA MTU SIKU YA MWISHO BABAKO ANAKUKANA UTAMMALIZA???

Bwana Samson Mfalila,

Watu wenye mawazo kama yako ndiyo wanaoleta chokochoko kwenye jamii na nadhani ndiyo wanaostahili kushughulikiwa ipasavyo. Kwani unahusisha kitua ambacho hauna uhakika nacho na kauli ya Mheshimiwa Rais, bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

Kwa kauli kama yako na maandishi kama yako katika jamii ya watu wasioweza kuchambuwa mambo unaweza kuwa chanzo cha kupoteza amani na utulivu tulionao Tanzania, na watu kama wewe ndiyo wanastahili kushughulikiwa na Dola.

Usitumie tofauti zako binafsi kama zipo na Rais Kikwete na maneno aliyoyatumia katika mazingira tofauti katika kutafuta mtaji wa umaarufu humu ndani ya jamvi la Jamii Forums.

Namalizia kwa kuwapa pole Familia ya Prof. Mwaikusa, Mungu amlaze mahali pema peponi. Mwisho nato Rai kwa vyombo vya dola kama wamo humu ndani, basi wafuatilie wanaohusika na ujambazi huu wafikishwe mbele ya sheria. na kuwakamata wengine wote wanaofanya matendo ya kijambazi katika miji yote ya Tanzania.

Bwana Mfalila unataka kutuambia kuwa na yale Mauaji yaliyotokea katika kisiwa cha ziwa la Victoria yalikuwa na uhusianao na mambo ya kisiasa?
 
RIP Prof. J Mwaikusa, Inasikitisha sana kusikia mtu ametolewa uhai wake just like that! Poleni wafiwa

Sijui ni kumbukumbu zangu au ndio uzee wenyewe.... kuna wakili mmoja aliuawa miaka michache iliyopita kwa staili hiyo hiyo, halafu sijui ni mwaka jana ule ambapo msomi mwingine toka UDSM aliuawa kwa staili ile ile.. (jina limenitoka kidogo) na sasa Mwaikusa. Aidha hawa "majambazi" wanapenda sana wasomi tena mawakili.. au

Mkj nafikiri huyo lawyer ni somebody Kapinga kama sikosei.
 
Back
Top Bottom