Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 12,001
- 27,175
Wakuu,
Akihojiwa na waandishi wa habari siku chache baada ya kuachiliwa na polisi kwa dhamana, wakili Mwabukusi amenukuliwa akisema."
Nataka nimwambie wazi IGP hatukuogopi, upo hapo kikatiba na kisheria, ukitaka siasa vua magwanda,toka kwenye bunduki njoo jukwaani." Hoja zetu za kisiasa anajibu kwa bunduki akiwa nyuma ya ofisi za umma, amevaa magwanda ya kiaskari? Alisema.
Aache watujibu, tunauliza maswali ya kitaaluma.
Pia amekemea Viongozi waliojigeuza miungu watu, nanukuu;
"Nchi hii kuna watu wamejigeuza miungu watu, wao na familia zao wanataka kugeuza watanganyika kama ngo'mbe wao zizini, watuswage kwenda machungani na kuturudisha muda wanaotaka. Nataka kuwaambia kama walifikiri sisi ni makondoo tumeshageuka kuwa wanambuzi wakorofi na tumeshanyanyua mkia kama ngiri na hawatatufuga tena.
Wanajificha kwenye kichaka mara waseme mapinduzi,sijui uhaini,mara waseme udini, kote huko ni kukwepa kuwajibika, sasa wanataka kupeleka sheria ya hovyo bungeni ili kujusfy IGA, na hii tunawaambia wabunge that luxury is long gone, na kwa sababu tulishaenda Mahakamani na mahakama ikasema haina uwezo wa kuingilia mambo ya bunge, hatutaenda mahakamani tena, tutatumia nguvu ya umma kuleta uwajibikaji, we will not go to court again, we do not have that time.
Ajabu,wanang'ang'ana na sisi tunaodiclose ubovu wa mkataba wanayaacha majizi na majitu yaliyolileta hapa taifa, yanakula na kutafuta vitumbua kwenye ofisi za umma, halafu unakimbizana na bonafide person ambaye anakwambia kuna shida mahali?
Kwahio ndugu zangu narudia kusema tena,IGA ni uvamizi wa taifa letu kiuchumi, bandari ni lango kwa taifa letu, bandari ni urithi tuliopewa na Mungu. Hatuwezi kuwa taifa la ubwege kiasi hiki, mbuga za wanyama tumewapa wageni, nenda kule,unaingia unaambiwa 'now you are entering the United Arab Kingdom' ndani ya nchi?
Tizama mahoteli yanayojengwa Ngorongoro pale,huku wamasai wakifurushwa kama wanyama kutoka kwenye ardhi yao,leo unataka kuniambia Mwarabu ndio ana Ikolojia ya Ngorongoro kuliko Mmasai? That is stupid aspect.
Halafu tukisema,watu wanasema wachochezi. Jamani hili taifa ni kwa ajili yetu,sisi hatujawekwa hapa kuwa watumwa na watwana wa wageni, tuna haki ya kufaidi fursa za kijamii, kiuchumi na kimaendeleo pamoja na kuzimiliki.
Kwahio, ndugu zetu mtuelewe, IGA sio nchi kwahio kuupinga haiwezi kuwa uhaini, IGA ni limkataba korokocho lililookotwa huko kizembe, watu wakafanya copy and paste wakifiri sisi ni mazuzu, tumelikataa."