Wakili Mwabukusi: Mkataba wa Bandari ni wa Kijambazi na Uvamizi dhidi ya Tanzania
Wakili Boniface Mwabukusi amesema wao kama Wanasheria hawatoruhusu Mikataba ya Kijinga, Wizi, Ufisadi na isiyo ya Kizalendo ikiwemo kuwepo Viongozi ambao wanatoka waziwazi na kushangilia Wizi na kuongeza kuwa Mkataba wa Ushirikiano wa Dubai na Tanzania ni wa Kijambazi.
Amewambia Mawaziri Nape Nnauye na Masauni kuacha kutoa kauli za hovyo na hawaogopi na anajua yeye ni kati ya watu ambao kauli zao zinawalenga.