Wakili Mwabukusi: Ninapotekeleza jukumu langu usinitishe, hatutakuogopa tutatekeleza wajibu

Wakili Mwabukusi: Ninapotekeleza jukumu langu usinitishe, hatutakuogopa tutatekeleza wajibu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876


Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi amesema hayo tarehe 30 Aprili 2026 wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu uliofanyika AICC jijini Arusha.​

Anasema TLS vilevile inawajibu mkubwa si tu kwa wanachama wake bali pia kwa jamii, serikali na mahakama katika kuhakikisha haki inatendeka, sheria zinaheshimiwa na misingi ya utawala bora inalindwa.

Na hapa ndipo pamekuwa pakionekana pana matatizo. Wengi hawaamini labda ukinipa gari au ukanijengea mfumo hauamini kwamba ninatakiwa nisimamie wajibu wangu wa kisheria.

Hatufanyi biashara ya kuuza wajibu tunatekeleza wajibu. Hapa ndipo penye kazi kubwa sana ambayo TLS tumekuwa tukiipata changamoto hususani sisi viongozi kwa sababu kuna baadhi wanashindwa kuelewa kwamba jukumu letu ni la kisheria.

Kwa hiyo ninapotekeleza jukumu langu usinitishie. Ukikamata mtu ukamfikisha mahakamani mimi nikaja kumsaidia tukampa legal aid usimshambulie wakili wala kutisha TLS kwa sababu hatutakuogopa tutaendelea kutekeleza wajibu wetu ukitaka tusifanye futa kifungu hicho cha sheria.

Na ndio jibu ambalo tumekuwa tukiwapa wenzetu kwamba hatufanyi sisi hatutetei mhalifu wala hatusemi huyu mtu asikamatwe lakini mtu akiomba huduma za msaada wa kisheria ni wajibu wetu kumpa kama anakidhi vigezo.

Tusidhibiwe kwa hilo limekuwa changamoto kubwa ambalo limeendelea na hali inakuwa sio nzuri imefika mpaka kuna mazingira watu wanaandika barua mahakamani wanaiondoa TLS haki yake au wajibu wake wa kutoa legal aid eh kwa sababu mbalimbali mtu anaandika barua unamuuliza unaondoaje haki ya kisheria au wajibu wa kisheria kwa barua lakini mtu anakuambia ndio siasa mmetaka siasa tumeingia kwenye siasa.

Kwa hiyo tunachojaribu kuonyesha kwamba members tujue kwamba licha ya maendeleo mazuri tunayopata kuna changamoto.


View: https://www.youtube.com/watch?v=dWCWnW9Kg3s
 
Back
Top Bottom