Wakili Nasoro Katuga hana papara ni very professional

hii kesi inaenda kuwa ya kihistoria
 
Nadhani pia atakupiga miti hivyo hivyo kiprofessional mahaluni wewe
 
Katuga: Kikao cha 3/4/2025 kati ya aina zile 4 za vikao chenyewe kinaangukia kwenye kikao kipi?

Golugwa: Hakipo kati ya vile vinne ila ulikuwa Mkutano wa ndani wa chama.

Katuga: Mkutano ulikuwa wa kikatiba?

Golugwa: Ndio kwasababu katiba yetu inaruhusu viongozi kukutana na wanachama

Katuga: Wewe ndio ulimwalika Lissu aje kuongea na watia nia?

Golugwa: Sahihi

Katuga: Wewe ndiye uliyemwandikia Hotuba?

Golugwa: Hapana sikumwandikia hotuba

Katuga: Je alikupa Hotuba yake kabla hajaja kwenye kikao?

Golugwa: Hapana hakuweza kunipa hotuba yake

Katuga: Je ulikuwa unajua alichofikiria kichwani mwake?

Golugwa: Wewe wakili unaweza kuingia kwenye kichwa cha mtu? Mimi nilikuwa najua anachoenda kukisema ambacho ni msimamo wa chama

Katuga: Nani alikuwa mwenyekiti wa huo mkutano?

Golugwa: Haukuwa na mwenyekiti

Katuga: Nani alikuwa mgeni rasmi?

Golugwa: Hakukuwa na mgeni rasmi

Katuga: Nani alikuwa wa mwisho kuongea?

Golugwa: Nilikuwa mimi

Katuga: Nani alikuwa wa mwisho kutoa hotuba?

Golugwa: Mwenyekiti wa Chama Tundu Lissu

Katuga: Nani aliongea kwa muda mrefu zaidi?

Golugwa: Mwenyekiti wa Chama Tundu Lissu

Katuga: Nani alikuwa amebeba dhima nzima ya mkutano huo?

Golugwa: Viongozi wote

Katuga: Wakati Lissu anaongea kulikuwa na vyombo vya habari?

Golugwa: ndio vilikuwepo

Katuga: Je Sekretarieti ilimlazimisha Tundu Lissu kuongea na vyombo vya habari?

Golugwa: Haikumlazimisha

Katuga: Je Lissu alitaka hotuba yake iende kwa umma?

Golugwa: Ndio alitaka

Katuga: Je alitaka hotuba ile iende kwa umma wa Watanzania?

Golugwa: alitaka
 
Naona amewatumia mashahidi wa mshitakiwa kumkaanga zaidi.
Hii kesi ni kesi ngumu na bora kwa rejea za mahakama
 
Kumbe wewe hii ndio picha yako?
 
Heche amekuwa mdogo mbele ya Katuga
 
Leo Katuga kawaachia taharuki wazee wa mabadiliko
 
Chai
 
Pia ni mtu mwenye uungwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…