DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema kuwa changamoto ya kupata Katiba mpya inachangiwa na watu wachache wanaonufaika na mifumo iliyopo na hivyo kuona mabadiliko kama tishio kwa masilahi yao binafsi.
Akizungumza na mtangazaji Wilberforce Ngoto katika kipindi cha Maswali na Majibu cha Jambo TV, Olengurumwa meinukuu kauli za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akieleza kuwa mara nyingi wanaopinga mabadiliko ni wale wanaofaidika na mifumo ya sasa kwa sababu ya tabia zao za kinyonyaji.
“Hata Mwalimu Nyerere alisema mtu yeyote ambaye anaendelea kufaidika na mifumo tuliyonayo, hawezi kuona umuhimu wa kubadilisha. Watu wote wanaoogopa mabadiliko ni wanyonyaji. Hatuwezi kupata Katiba mpya ikiwa bado wapo wanaokwamisha maboresho kwa sababu kufanya hivyo kunatishia mirija yao na masilahi yao,” amesema Olengurumwa.
Ameongeza kuwa mfumo wa kidemokrasia, vyama vingi, asasi za kiraia na vyombo vya habari ni nyenzo muhimu za mabadiliko, lakini changamoto kubwa inabaki kuwa vizingiti vinavyowekwa na wachache wenye maslahi binafsi.