Wakili Paul Kaunda: Mawakili tulindwe tunapotekeleza wajibu wetu

DodomaTZ

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
84
Reaction score
118
Wakili Paul Kaunda amesema ameamua kugombea nafasi ya Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa Mwaka 2024, sababu anataka kuwalinda na kuwatetea Mawakili wachanga ili aongeze thamani na heshima.

Ameeleza kuwa Mawakili wachanga wapo takribani 60% na kutimiza hilo taanza kwa kuwatengenezea Wakili APP ambayo itasaidia wapate Wateja kwa urahisi na kupata malipo stahiki kwa mujibu wa Sheria ya gharama za Mawakili.

photo_2024-07-28_17-39-48.jpg

Amesema “Lengo ni kuongeza soko la upatikanaji wa huduma kwa mawakili hasa mawakili wachanga ambao wanashindwa kupenya kwenye legal market kutokana na kutawaliwa sana na mawakili maarufu, pia kuwasaidia Mawakili Vijana, mfano walioapishwa juzi wapo 555, je wanapataje Wateja?”

Ameeleza kuwa atamshauri na kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutunga Kanuni zitakazotulinda Mawakili na kuwaheshimisha wanapofanya majukumu yao Mahakamani, Polisi na kwingineko.

Ameongeza “Nitamshauri na kumshirikisha Jaji Mkuu wa Tanzania aone umuhimu wa kuanzisha Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Teknolojia, kwasasa Dunia ipo kwenye mapinduzi ya nne ya Viwanda na wengine wanasema inakwenda kwenye mapinduzi ya tano ya viwanda, tuandae Mahakama ambayo itahusika na mambo yaliyojitokeza kwenye teknolojia ikiwamo Akili Mnemba, nitashauri shule na Vitivo vya sheria kuboresha mitaala yao ya sheria iendane na mapinduzi ya nne ya viwanda ili wahitimu wapambane na nguvu ya soko.”

Amesema “Kwa muda mrefu Mawakili tumekuwa tukidharauliwa na Vyombo mbalimbali vya Kisheria, tutamshauri ili Mawakili tulindwe tunapotekeleza wajibu wetu katika sehemu mbalimbali za utoaji haki.”

Amesema wataboresha tuzo mbalimbali za Wanasheria na kusimamia weledi wa hali ya juu mchakato wa Katiba Mpya kwa kuishauri Serikali ili uendelee kupata katiba bora kwa Wananchi kwa haraka ambayo itakuwa ni matakwa ya Sheria.

Ameeleza kuwa wasifu wake wa kufanya kazi ya Uwakili kwa zaidi ya Miaka 10 katika maeneo mbalimbali ya Sheria kuanzia Mahakama ya Mwanzo hadi Mahakama ya Rufani, Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki , Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu anaamini vinamfanya awe mtu sahihi wa nafasi hiyo.
 
We stand with Mwakubusi.
Waliomuwekea pingamizi ndio wamemuongezea umaarufu.
Yule mwamba hajapandikizwa na serikali.
 
Wakili Paul Kaunda amesema ameamua kugombea nafasi ya Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa Mwaka 2024, sababu anataka kuwalinda na kuwatetea Mawakili wachanga ili aongeze thamani na heshima.

Ameeleza kuwa Mawakili wachanga wapo takribani 60% na kutimiza hilo taanza kwa kuwatengenezea Wakili APP ambayo itasaidia wapate Wateja kwa urahisi na kupata malipo stahiki kwa mujibu wa Sheria ya gharama za Mawakili.

View attachment 3055237
Amesema “Lengo ni kuongeza soko la upatikanaji wa huduma kwa mawakili hasa mawakili wachanga ambao wanashindwa kupenya kwenye legal market kutokana na kutawaliwa sana na mawakili maarufu, pia kuwasaidia Mawakili Vijana, mfano walioapishwa juzi wapo 555, je wanapataje Wateja?”

Ameeleza kuwa atamshauri na kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutunga Kanuni zitakazotulinda Mawakili na kuwaheshimisha wanapofanya majukumu yao Mahakamani, Polisi na kwingineko.

Ameongeza “Nitamshauri na kumshirikisha Jaji Mkuu wa Tanzania aone umuhimu wa kuanzisha Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Teknolojia, kwasasa Dunia ipo kwenye mapinduzi ya nne ya Viwanda na wengine wanasema inakwenda kwenye mapinduzi ya tano ya viwanda, tuandae Mahakama ambayo itahusika na mambo yaliyojitokeza kwenye teknolojia ikiwamo Akili Mnemba, nitashauri shule na Vitivo vya sheria kuboresha mitaala yao ya sheria iendane na mapinduzi ya nne ya viwanda ili wahitimu wapambane na nguvu ya soko.”

Amesema “Kwa muda mrefu Mawakili tumekuwa tukidharauliwa na Vyombo mbalimbali vya Kisheria, tutamshauri ili Mawakili tulindwe tunapotekeleza wajibu wetu katika sehemu mbalimbali za utoaji haki.”

Amesema wataboresha tuzo mbalimbali za Wanasheria na kusimamia weledi wa hali ya juu mchakato wa Katiba Mpya kwa kuishauri Serikali ili uendelee kupata katiba bora kwa Wananchi kwa haraka ambayo itakuwa ni matakwa ya Sheria.

Ameeleza kuwa wasifu wake wa kufanya kazi ya Uwakili kwa zaidi ya Miaka 10 katika maeneo mbalimbali ya Sheria kuanzia Mahakama ya Mwanzo hadi Mahakama ya Rufani, Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki , Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu anaamini vinamfanya awe mtu sahihi wa nafasi hiyo.
Sasa hivi mpango mzima ni Shia Islam.

Allah ampe qauli thabeet kipenzi chetu Imam Hussein.
 
Back
Top Bottom