Wakili Paul Kisabo: Lissu atamuhoji Kamishna Mkuu wa Magereza "Shauri la Kimkataba"

Wakili Paul Kisabo: Lissu atamuhoji Kamishna Mkuu wa Magereza "Shauri la Kimkataba"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, anatarajiwa kuwahoji kwa maswali ya dodoso (cross-examination) Kamishna Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga katika Shauri la Kikatiba Namba 7300 la Mwaka 2026 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma.

Katika mahojiano maalum na ya moja kwa moja na Sasa Live leo Juni 30, 2026, jijini Dar es Salaam, mmoja wa mawakili waliofungua shauri hilo, Wakili Paul Kisabo, amethibitisha kuwa mnyukano huo wa kisheria utaanza kesho Julai 1 hadi Julai 3, 2026. Shauri hilo litasikilizwa kwa njia ya mtandao (online) mbele ya jopo la majaji watatu; Mhe. Jaji Mruma, Mhe. Jaji Dkt. Rumisha, na Mhe. Jaji Dkt. Longopa.

Shauri hilo lilifunguliwa na mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu, na Paul Kisabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza, na Mkuu wa Gereza la Ukonga, wakiiomba mahakama kuamua kuhusu ukiukwaji wa misingi ya kikatiba gerezani.

Wakili Kisabo amebainisha kuwa miongoni mwa mambo makuu yanayolalamikiwa ni pamoja na viongozi na wanachama kuzuiwa kumuona Lissu, pamoja na vitendo vya askari magereza vya kusikiliza mazungumzo ya siri kati ya mwanasiasa huyo na mawakili wake wanapofanya mashauriano ya kisheria—jambo linalokiuka haki ya faragha.

Katika shauri hili, Tundu Lissu ametajwa kama mmoja wa wajibu maombi (Respondents), huku Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kikishiriki kama mdau mwenye maslahi katika shauri (Interested Party) baada ya mahakama kukubali maombi yao.

Kutokana na uzoefu wa changamoto wanazokumbana nazo wanapomtembelea kiongozi huyo, Lissu anatarajiwa pia kuwahoji mawakili wake wenyewe waliofungua shauri hilo ili waieleze mahakama mazingira halisi ya utendaji kazi wao.

Wataalamu wa sheria wanaona shauri hili kama miongoni mwa mashauri muhimu zaidi ya kikatiba nchini, ambalo linaweza kuweka mwelekeo mpya wa kisheria kuhusu haki ya mawakili kufanya mashauriano ya faragha na wateja wao waliopo magerezani au mahabusu, pamoja na kulinda usiri wa mawasiliano yao.
 
Mihimili yote imebakwa na Kulawitiwa.

Hakuna
Bunge wala Mahakama.
 
Back
Top Bottom