Wakili Peter Kibatala, azitaka mamlaka za usalama nchini kutoa hali ya usalama ya Polepole inajulikana na kuwekwa wazi kwa umma

Wakili Peter Kibatala, azitaka mamlaka za usalama nchini kutoa hali ya usalama ya Polepole inajulikana na kuwekwa wazi kwa umma

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wakili maarufu Peter Kibatala, ametaka mamlaka za usalama nchini Tanzania kutumia rasilimali zote kuhakikisha hali ya usalama wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole inajulikana na kuwekwa wazi kwa umma, kufuatia taarifa zinazodai kuwa mwanasiasa huyo ametekwa.

Kupitia taarifa yao kwa umma iliyotolewa Oktoba 6, 2025, mawakili wa Polepole wakiwakilishwa na Kibatala wameeleza kuwa mteja wao amewahi kuhudumia taifa katika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa umma, hivyo ni muhimu mamlaka kutoa taarifa rasmi kwa Watanzania na jumuiya ya kimataifa kuhusu usalama wake.

“Tunazitaka mamlaka za usalama wa raia na mali zao kutumia mbinu na rasilimali zote za umma kuhakikisha, na kisha kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania, na dunia kwa ujumla juu ya hali ya usalama, na maslahi ya kisheria ya Balozi [mstaafu] Humphrey Polepole”, imeeleza taarifa hiyo.

Pia Soma:



Amesema wataendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu hatua wanazochukua kwa kushirikiana na watu na taasisi mbalimbali duniani kote, ili kuhakikisha suala hilo linapata majibu ya wazi.

Tamko hilo limekuja muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi kutangaza kuwa linaendelea kufuatilia taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa Humphrey Polepole ametekwa, huku likieleza kuwa bado linamsubiri aripoti kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma alizozitoa mtandaoni.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Polepole alitumiwa barua ya wito kwa mujibu wa sheria kuhojiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), lakini hadi sasa hajatekeleza maelekezo hayo.
 
Kama rasilimali zote zikitumika kwa ajili ya Polepole pekee na sisi wengine tutatumia rasilimali gani?
 
Hapa ndipo tunapofel wabongo Yan mtu aliyetekwa na wasiojulikana unaenda kumtafuta kwa kutumia sheria😏😏
 
Back
Top Bottom