Wakili Peter Madeleka afunguliwa mashtaka matano ya dharau kwa mahakama (Contempt of Court)

Wakili Peter Madeleka afunguliwa mashtaka matano ya dharau kwa mahakama (Contempt of Court)

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,628
Reaction score
6,818
DAR ES SALAAM: Jamhuri imemfungulia mashtaka matano ya dharau kwa mahakama (Contempt of Court) Wakili Peter Michael Madeleka (46) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mashtaka hayo yanahusiana na kauli na machapisho anayodaiwa kuyatoa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya mtandaoni kuhusu shauri la kiuchumi linaloendelea Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani hapo Agosti 20, 2026, Madeleka anakabiliwa na makosa manne chini ya Sehemu ya 114 (1) (a) na kosa moja chini ya Sehemu ya 114 (1) (d) ya Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16 Rejeo la 2023).

Shtaka la Kwanza hadi la Tatu (Dharau kwa Mahakama): Yote yamefunguliwa chini ya Sehemu ya 114 (1) (a) ya Kanuni ya Adhabu. Mshtakiwa anadaiwa kutoa na kuchapisha hotuba kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya mtandaoni, ikiwemo Jambo TV, tarehe 27 Julai 2026 na 28 Julai 2026 (eneo la Mawasiliano, Ubungo) pamoja na tarehe 07 Agosti 2026 (Mikocheni, Kinondoni).

Vitendo hivyo vinadaiwa kuonyesha ukosefu wa heshima dhidi ya amri iliyotolewa na Jaji Mfawidhi Julai 27, 2026, kwenye Kesi ya Kiuchumi Namba 4521 ya 2026 (Jamhuri vs. Wendy William Ishengoma na Wenzake Waane) inayotajwa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Peremende/Uchumi.

Shtaka la Nne (Upotoshaji wa Mwenendo wa Mahakama): Linamkabili chini ya Sehemu ya 114 (1) (d) ya Kanuni ya Adhabu. Anadaiwa mnamo Agosti 07, 2026, eneo la Mikocheni, kutoa maelezo ya uongo na kupotosha mwenendo wa shauri hilo kwa kudai kuwa: "Mawakili wa Serikali walikuwa wanaomba vielelezo vilivyotolewa mahakamani vikahifadhiwe kwenye ofisi ya Taifa ya Mashtaka...", kauli ambayo upande wa mashtaka unadai alijua ni ya uongo.

Shtaka la Tano (Dharau kwa Mahakama): Chini ya Sehemu ya 114 (1) (a) ya Kanuni ya Adhabu, Madeleka anadaiwa mnamo Agosti 13, 2026, katika Wilaya ya Ubungo, kutoa na kuchapisha tena hotuba kwenye mitandao inayokiuka amri hiyo ya mahakama ya Julai 27, 2026.

IMG_7346.jpeg
IMG_7347.jpeg
IMG_7348.jpeg
 
Back
Top Bottom