Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Mwanaharakati na mwanamitandao maarufu nchini Martin Maranja Masese amedokeza Wakili maarufu Tanzania Peter anashikiliwa na Jeshi La Polisi.
Wakili Madeleka anashikiliwa na Central Police - Dar es Salaam kwa tuhuma za makosa ya mtandao ambayo hajaelezwa. Mapema leo aliitwa polisi kwamba akajadiliane na ZCO katika shauri lake lingine na mteja wake, alipofika amehojiwa kwa makosa ya mtandao. Peter, amenyimwa dhamana.
Ikumbukwe kwa muda mfupi kabla ya taarifa hii kutoka kwa Martin, Madeleka kupitia akaunti ya X alidokeza kuwa aliitwa kituoni na ZCO wa Dar Es Salaam, Faustine Mafwele kwa ajili ya Mashauriano