Hii imenishtusha sana.
Wakili amekwenda kumtembelea mheshimiwa Mbowe huko jela, na cha ajabu amewekwa sehemu ambayo hukaa wafungwa wanaosubiri kunyongwa. Mheshimiwa Mbowe hajahukumiwa mahakama yoyote lakini anakuwa treated vibaya sana.
Kwa kweli huu ni ukatili usio na kifani.
Kosa la mheshimiwa Mbowe ni kudai katiba mpya tu, kitu ambacho kimsingi kipo kwa mujibu wa sheria, maana kuna sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012.
Kwa kweli sikudhani kuwa serikali hii ingekuwa katili kiasi hiki.
But hebu ngoja tuone mwisho wake.
-----------------------------------------------------
Anaandika Wakili Peter Madeleka
Serikali ya SSH inafanya mambo yasiyokubalika kwa Freeman Aikael Mbowe.
Nilienda gereza la Ukonga na kwa bahati mbaya Sana nilikataliwa kumuona Mbowe Ingawa ninafahamika mimi ni wakili na nimeenda pale kwa mambo ya kisheria.
Kitu Cha ajabu imetolewa amri kutoka sehemu fulani na uongozi wa magereza umemtenga Mbowe na mahabusu wenzake na badala yake amewekwa pamoja na wafungwa wanaosubiri kunyongwa
Hii haikubaliki na ni Lazima kila mtu apige Kelele kwa anachofanyiwa Mbowe
View attachment 1928334