JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Katika shauri hilo, upande wa mlalamikaji uliomba Mahakama kutoa amri ya kukamatwa kwa mtuhumiwa na kufikishwa mahakamani. Hata hivyo, Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Nyamburi Tungaraja, ameeleza kuwa si jukumu la Mahakama kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha mahakamani. Uamuzi huo ulizua maswali zaidi, hasa baada ya upande wa washtakiwa kutohudhuria mahakamani siku hiyo.
Baada ya kikao hicho cha Mahakama, Wakili wa mlalamikaji, Peter Madeleka, amezungumza na wanahabari na kueleza nia yake ya kupeleka maombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, ili kufuatilia na kupitia mchakato mzima wa uendeshaji wa kesi hiyo. Wakili Madeleka amedai kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa sheria katika usikilizwaji wa shauri hilo.
Wakili huyo pia ametoa malalamiko kuhusu kitendo cha Hakimu Tungaraja kumfokea mahakamani, jambo ambalo aliliona kama kukosewa heshima mbele ya Mahakama, na amekusudia kumpeleka Hakimu huyo kamati ya maadili kwa kitendo alichodai kukifanya.
Madeleka amedai kuwa hana imani tena na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma na kwamba kutokana na mazingira hayo, hawaoni haja ya kuendelea na shauri hilo mbele ya Mahakama hiyo.
Ingawa kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 16, 2024, upo wasiwasi kuhusu mwenendo wake kutokana na malalamiko ya upande wa mlalamikaji kuhusu kutotendewa haki.
Stori: Jambo TV (Oktoba 15, 2024), Video: Global TV