Wakili Peter Madeleka: Mimi na mke wangu tulikamatwa na kushtakiwa kwa uhujumu uchumi, nitawashtaki

Hao ni mashetani katika maumbile ya wanadamu. Hawana tafakari kama hiyo ya kwako juu watoto na haki za hao wanaowaonea. Hao kwa tafsiri sahihi ndiyo magaidi, maana dhamaira yao ni kuleta terror ili maovu yao yasihojiwe na yeyote.
 
Huyu wakili kufanya KAZI polisi na mke wake pia kua afisa wa uhamiaji lazima kuna mgongano wa kimaslahi maana chocho zote za kuwatetea wahamiaji haramu wanajua.

Kuna kitu kaficha
Hakuna cha kuficha. Kama angekuwa ametenda uovu, wasingemwachia.
 
Umesoma lakini inaonekana umetoka zero.

Yeye ameishtaki Serikali kwa kumweka mahabusu bila hatia. Lakini ili atoke ilimlazimu akiri kosa na alipe milioni 2.

Kwa hiyo serikali ushahidi itakaoutumia dhidi yake ni kukiri kosa. Upenyo alionao ni kukiri kwake kosa kufutwe kwa sababu hakukufuata utaratibu. Kukiri kwake kosa kusipotambulika kwa vile hakukufuata utaratibu, basi sasa atakuwa na haki ya kulalamikia tendo la yeye kuwekwa mahabusu bila hatia, na baadaye kufutiwa mashtaka kwa kukosa ushahidi.
 
Inaonekana watu mbalimbali walikuwa mahabusu kwa uonevu kutokana na Magufuli. Yeye tu kufariki tarehe 17 Machi, tarehe 30 Machi hiyo hiyo, akaachiwa.

Mwanadamu hufurahii kifo cha binadamu mwenzako, lakini kifo cha Magufuli kimewaokoa wengi kutoka kwenye mateso na dhuluma mbalimbali.
 
Wewe ulikua mtumishi hewa ulifoji cheti huna lolote
 
Wewe ulikua mtumishi hewa ulifoji cheti huna lolote
Kama mm nilofoji vyeti wewe itakuwa uliviandika kwa mkono! Nifoji vyeti kwann? Weka hapa vya kwako nami niweke tuone nani kafoji.
 
Nashukuru kwa sifa uliyonipatia, ila uelewe hawa mawakili ni wajanjawajanja sana, kwani si amesema mwenyewe alikuwa anawatetea hata waharifu?
 
Bila shaka amewagusa wenye nchi inasikitisha sana kwakweli.
 
Angenyamaza tuu.. ...

Watamuondoa ... ...

Haya sasa.. ...
 
Bila shaka amewagusa wenye nchi inasikitisha sana kwakweli.
Kila mtu anamambo yake ambayo asingependa yajulikane, changamoto inakuja unafanya maovu ila unajificha kwenye mgongo wa siasa mwisho wa siku ukikamatwa unawapa wafuasi wako mwanya waitengeneze hiyo issue kuwa yakisiasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwan wapi imesemwa ni issue ya kisiasa? Huyo kagusa maslahi ya watu wazito hasa huko uhamiaji.
 
Nilijua, hii ya leo sio mara ya kwanza huyu jamaa kukamatwa.
 
Angenyamaza tuu.. ...

Watamuondoa ... ...

Haya sasa.. ...
Huyu jamaa anaongea sana na ukifuatilia sana utakuta kuna baadhi ya mambo anaforce sana.

Angepiga kimya tu. Kuna kitu alikua anakitafuta na kakipata.
 
21 April 2022

WAKILI WA PETER MADELEKA AIBUA MAZITO KINACHOENDELEA BAADA YA KUKAMATWA KWA WAKILI PETER MADELEKA


Source : Mubashara Studio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…