Mkuu naona leo umevurugwa[emoji3][emoji3].Mimi kwa taarifa yako naamini kabisa Mbowe kwa mashtaka yale kuna walakini,lakini najaribu pia kujizuia na kuangalia uhalisia wa kinachoendelea Mahakamani,maana tayari ni kesi inaendelea,siwezi kupeleka hisia zangu kumtukana mtu kisa ameitwa kutoa ushahidi tena kwa nafasi yake.Ndiyo maana kina Kibatala wako pale kupigania haki ya Watuhumiwa,hawajasusa kisa tu wanajua haya ni mashtaka ya kutengenezwa.
Lakini pia huoni kama pengine kupitia huyu shahidi ndiyo ku naweza patikana mianya mingi ya kuwasafisha Watuhumiwa? Assume ushahidi ungeishia kwa Kingai peke yake,wewe ungejuaje weakness za kesi hii?
Unaweza kuta huyu shahidi pia ni mfuasi mzuri tu wa Mh.Mbowe,lakini hapo alikuwepo kutekeleza wajibu wake.Naamini hata wewe ungeitwa kwa nafasi ya Cheo chako usingegoma kwenda Mahakamani,it’s easier said than done.Otherwise nakuelewa sana tu.