Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Huku marufuku ya TikTok ikikaribia, wanasiasa wa Marekani wanaoendelea kupinga China wamegundua kwamba App nyingine ya kijamii ya China ‘Rednote’ imezidi kuwa maarufu nchini Marekani. Katika siku za hivi karibuni, idadi kubwa ya watumiaji wa TikTok wa Marekani wamejiunga na Rednote, na kuwasiliana kwa karibu na wanamtandao wa China. Wamarekani hao wamefahamu kuwa hali halisi ya China ni tofauti sana na ile waliyoambiwa na serikali na vyombo vya habari, na Rednote imewafungulia dirisha jipya la kuifahamu China.
Rednote iliyoanzishwa mwaka 2013, hivi sasa ina watumiaji takriban milioni 300, na imekuwa moja ya mitandao ya kijamii inayopendwa zaidi nchini China.
Katika siku za hivi karibuni, watumiaji wa Rednote ghafla wamegundua kuwa kuna Wamarekani wengi waliojitokeza kwenye App hiyo ya China.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Marekani, Rednote imeshika nafasi ya kwanza kati ya APP zilizopakuliwa zaidi nchini Marekani katika siku chache zilizopita.
Watumiaji hawa wa TikTok wa Marekani walichapisha picha na video zao za maisha kwenye Rednote, na wanajiita “wakimbizi wa TikTok kutoka Marekani”. Wameeleza kuwa madhumuni yao ya kuhamia Rednote ni kulalamikia uamuzi wa serikali ya Marekani kupiga marufuku TikTok.
Licha ya hayo, wanamtandao wa Marekani wameshangaa kwamba, kwa kuwasiliana na wanamtandao wa China kwenye Rednote, wamegundua dunia mpya, na kufahamu kuwa China ni tofauti kabisa na walivyofikiria. Kwa watu wa Marekani, ni kweli kwamba China ni nchi ya mbali sana, na utamaduni wa Kichina ni tofauti kabisa, na katika miaka ya hivi karibuni, China imejulikana kama “tishio kubwa zaidi” la Marekani.
Lakini ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinadai kuwa, Wachina wanaishi maisha magumu na kukandamizwa sana na serikali.
Kwenye Rednote, Wanamtandao wa Marekani wanaweza kuzungumza na Wachina wa kawaida moja na moja, na wamebadilishana habari mbalimbali kuhusu maisha, kutoka kipato hadi bima ya matibabu, kutoka chakula hadi mfumuko wa bei, kutoka masuala ya burudani hadi wanyama vipenzi. Wamarekani hao wamegundua kwamba kumbe Wachina wanaisha maisha furaha sana.
Matibabu ni moja ya mada motomoto zinazojadiliwa kati ya wanamtandao wa China na wa Marekani, na makundi ya bima ya matibabu nchini Marekani yanalalamikiwa sana katika miaka ya hivi karibuni.
Wakati huohuo, wanamtandao wa Marekani wameshangaa sana baada ya kujua kwamba Wachina wanapata huduma nzuri za matibau kwa kulipa makumi ya dola za Kimarekani kwa mwaka. Zaidi ya hayo, bei za dawa nchini China ni nafuu sana.
Kwa mfano, chupa ya insulini inayoweza kutumiwa kwa wiki mbili inagharimu chini ya dola mbili nchini China, huku wagonjwa wa kisukari nchini Marekani wakitumia angalau dola 6,000 kila mwaka kwa matibabu ya msingi.
Kupitia Rednote, wanamtandao wa Marekani pia wamegundua kwamba magari ya nishati mpya nchini China yana bei nafuu na ya ubora wa juu ikilinganishwa na soko la Marekani, na watu wanaweza kununua aina tofauti za magari kulingana na uwezo wao wa kiuchumi.
Lakini wakati dunia nzima inanunua magari mazuri ya China, Marekani, ambayo inajidai kutetea “biashara huria na ya haki,” imeweka vikwazo vikali dhidi ya magari hayo.
Hali hii imegusa hisia za Waamerika wengi, ambao wanaona kwamba katika miaka ya hivi karibuni, China imeonesha uwezo mkubwa wa uvumbuzi na utengenezaji, na ikilinganishwa na China, Marekani inaonekana kama nchi ya dunia ya tatu.