Wakina mama kuweni na huruma jamani. Amezaa mtoto kaenda kumtupa porini

Wakina mama kuweni na huruma jamani. Amezaa mtoto kaenda kumtupa porini

Nyuma ya haya yote yupo mwanaume.....haijalishi kakosea au hajakosea
 
ata kama yupo mwanaume!! utamfanyiaje ukatili mwanao uliemtoa kwenye MAKU yako??
Haya angetokea puani ukiamua kufanya ukatili huchagui ni nani wa kumfanyia..... mbona nyie mnatokea huko na mnawaumiza kimakusudi na dharau juu
 
Kama mnyama asiye na akili anabeba ujauzito,anazaa,mpaka kutunza watoto peke yake kiugumu bila ya kujali aliyemtia mimba hakuwahi kumsaidia,sembuse wewe mwanadamu?,huyu ni mwanamke asiyefaa kwenye jamii,mwanamke huwa hatupi mtoto,hata ingekuwa kuna magumu ya kiasi gani,hapa hawezi kujitetea kwa lolote...
Mnyama anapitia bullying gani toka kwa ndgu na wazazi wake??

Ni jambo baya kutupa mtoto ila sio wana uwezo wa kustahimili manyanyaso na unyanyapaa.

Kwahiyo, pamoja na kulaani kitendo cha kinamama kutupa watoto ila na jamii ijue kupata mimba kabla ya ndoa, au shuleni sio kosa la kumnyanyapaa na kumtenga mtu.
 
Na Bado wakija JF Kila Kona utasikia single Maza hivi singo maza vile, basi tu ilimradi wasipate utulivu.

Si jambo zuri na siombei itokee, lakini likimkuta Binti yangu inabidi kusimamia nae Kwa kipindi chote. Wakati wa kuonyesha upendo wa dhati.
Ndo hivyo mkuu, hawahawa wanaowadisi singo maza humu ndo wazazi wa hao watoto.

Huyu anaembwatukia singo maza jf siku akishuhudia mwanae ni singo maza ajae lazima atamsakama tu.
 
Back
Top Bottom