Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii


Nitakujibu point zako kama ifuatavyo;

1. Kwanza tu tayar ni used out, you deserve better.
Mwanamke aliyezaa haina maana katembea na wanaume wengi zaidi ya yule ambaye hajazaa. Kwa hiyo huyo unaemtaka wewe ambae hajazaa anaweza kuwa used zaidi ya huyo aliyezaa. Na huyo ambae haja zaa, unajua historia yake? Vipi kama alikuwa anatoa mimba kila akipata? Labda basi tafuta bikira
2. Wamepitia maumivu sana na mamekua sugu, mda wowote yupo tayari kuvunja uhusiano.
Jibu na (1) hapo juu linahusika
3. Wanachuki dhidi ya wanaume waliowazalisha na kuwa dump. Subconciously wanachukia wanaume wote.
Kuna wanawake single mothers wamewa-dump wanaume waliozaa nao. Kwa hiyo si mara zote kwamba single mothers walikuwa dumped
4. Kubali uskubali hawez kua mwaminifu kwako, baba wa mtoto akitaka anakula tena kavu.
Kimsingi, hakuna tofauti kati ya wanawake wawili waliotembea na wanaume kabla yako na mmoja akazaa na mwingine hakuzaa. Kumbuka mimba mara nyingine ni ajali tu, na usiwe na mentality kwamba wanaopata mimba ndio wamekubuhu kwa ngono. In fact, mara nyingi wanaopata mimba za ajali wakazaa ni wale ambao hawajakubuhu kwa ngono. Unaweza ukafuata asiye na mimba kumbe alishazitoa zaidi ya mara tano. Pia, hata huyo ambae hakuzaa lakini alitembea na mwanaume fulani kabla yako anaweza kugawa tena kwa mwanaume alietembea nae huko nyuma. Hivyo ukitaka kuwa safe kwa karata hii tafuta bikira.
5. Atakuumiza tu hebu fikiria karuhusu kuachana na mwanaume tena waliopendanda ujanan vipi kuhus wewe
Point namba nne hapo juu inahusika. Kuzaa na mwanaume mwingine sio lazima kwamba alimpenda huyo kuliko wewe. Anaweza akawa hakuzaa lakini akawa bado anampenda mwanaume wake wa nyuma kuliko wewe

Kwa hiyo mwisho wa mambo yote Mkuu - If you want my future, forget my past
 
Duuh! Wapumzishe jamani hawa watu maana mtoa mada unawachukulia vibaya sana na unawahukumu kwa makosa ambayo sio yao kabisa, laiti ungejua sababu iliyopelekea kuwa hivyo naamini usingesema hayo
 
Nafikiri mleta uzi ana hoja ya msingi. Pia anajaribu kuwaamusha wanawake kutozaa na wanaume ambao sio waume zao.
Na hana tofauti na kauli ile ya kutosomesha wanafunzi wenye watoto
 
mimi nimempenda single mother ana miaka 21 mtoto mzuri wa kimburu nataka kumuoa pia aliachana na mpenzi wake wa zamani sababu alimsaliti na alikua mkorofi sanaa, bado nafanya research zaidi kwake ila nimetokea kumpenda hasa
 
Mkuu Andie, asante kwa ufafanuzi. Umeshahu point moja. Asilimia kubwa yao wanawaka tamaa. Yaani haoni tabu kuwa na mwanamme mpya kila mwezi. Yaani sijui wanakuaje. Yaani mwanzo anakuwa na mapenzi baada ya muda anamchoka mpenzi wake pasipo sababu.

Ushauri, wanaume naomba tuwaonee huruma. Kwani wanaume wanawachezea wanavyotaka sababu wanajua tabia zao. Wao malengo yao ni kupata mume wa kusaidiana maisha na Mwanaye apate wa kumuita baba. Ila wanaume wanalenga kumchoma na mwanaume atakayemheshimu humfanya nyumba ndogo. Naomba wanaume muwaoe tu. Wengi wakifika ndani ya ndoa hutulia na kuwaheshimu waume zao. Hawarudi tena nyumbani usiku wa manane wala hawalali nje. Hata starehe wanaacha wakishapata mtu anayemuweka ndani. Mungu awasaidie awaepushe na shetani anayewafanya wajione kichwa kigumu,kiburi na jeuri yaani yale mambo ya kwamba hawasikii la mjumbe wala mpiga adhana waache.
 
Ahsanteni
 
Swali
1.Single mother mtoto 1 au 2,3 ? Nafikiri kila mwanadamu anastahili heshima na kuthaminiwa utu wake pamoja na upendo.Kama Tabia ya mtu ni mbaya haiwezi kubadilika hata ukimpeleka akaishi ikulu ya marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…