Wakipitia kurasa zako za mitandao ya kijamii wakati wa usaili utapata kazi?

Wakipitia kurasa zako za mitandao ya kijamii wakati wa usaili utapata kazi?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Wakuu,

Kama tunavyojua na kama ulikua hujui basi uliweke akilini kuanzia leo, unachoweka mtandaoni hakifutiki, utasema nimedelete hakipo tena lakini ukweli ni kwamba kipo na kurudishwa ni sekunde tu.

Hivyo ni muhumu kuchukua tahadhari unapokuwa mtandauni, kichani ukumbuke kila unachofanya mtandaoni kinakuelezea wewe jinsi ulivyo na kinaweza kutumika dhidi yako kikakuharibia pakubwa.

Vitu unavyolike, comments unazoweka kwenye post mbalimbali, picha/video unazoweka bila kusahau captions zako zinaweza kukusaidia au kuharibia vibaya kwenye harakati zako za kusaka ugali.

Kuna story moja niliipata sehemu, kuna jamaa kipindi fulani alikuwa na kazi nzuri sasa kuna benki alikuwa haipendi, akaacha comment mtandaoni akiiponda ile benki vilivyo.

Siku ya siku alipokuwa anafanya kazi mkataba ukaisha akaenda kuomba kazi kwenye benki hiyo aliyoichamba. Usaili akafanya vizuri sana, yaani kazi ilikuwa yake, njia nyeupeee, si ndio wakamuonesha comment yake, wewe ulisema hivi kuhusu sisi, utawezaje kufanya kazi hapa kwa watu unaowachukia hivi? Na kazi ikapeperuka namna hiyo!

Tuwe makini kwa tunavyoweka, kulike na kucomment sababu hujui nani anakufatilia na fursa ipi unazuia.

Ulishawahi kukosa mchongo kutokana na hili? Una maoni gani kuhusu hili?

Kwenu Wakuu.
 
Back
Top Bottom