Wako wapi hawa wasanii?

Wako wapi hawa wasanii?

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
56,205
Reaction score
79,515
Umofia kwenu wana JF,

Ebwana nawaulizia hawa wasanii waliowahi kutamba miaka hyo kwenye fani ya music

1.Ras Pompidou mara ya mwisho kumuona ilikuwa kwenye Tamasha lililoandaliwa na Eastafrika Radio 98 aliimba wimbo wa kuisifu EAradio moja ya mashairi eita sevena pointa eita efema is mai choisa(in buju banton voice)

2.Jah Kimbuteh mara ya mwisho kumuona ilikuwa YMCA 93 pale uwanja wa basket alikuwa anatumbuiza tamasha

3.Mac Mooger huyu jamaa sijui yupo wapi nlisikia story zake kwa jamaa wa m/nyamala na kupitia kitabu cha sugu

Wapo wapi hao kwa sasa?
 
Mmh apa nimewahi kumsikia Mac mooger tu wengine ndo kwanza nakusikia wewe,ngoja waje
 
Pompidou alikuwa inafrika band sina hakina kama yupo mpaka leo maana band yenyewe imeshuka kimtindo...
 
Ebu dadavua huyo mtu,maana niliona kwenye kitabu cha sugu amemzungumzia kwamba ni msanii ambaye alianza kutoa album kabla yake yeye na pia ali kiba alimuimba huyo msela na ni true story baada ya mshkaji wangu wa m/nyamala kuniambia jamaa mac mooger alikuwepo na alikuwa mtu wa kujirusha sana!!
 
Hata Mimi nilimsikia kupitia nyimbo ya alikiba, nilijaribu kumtengeneza kwa kutumia fikra zangu alikuwa ni mtu wa aina gani na ni nani, kwa kifupi nilitaman kujua hostoria yake kwa ujumla ila nyimbo ilivyokufa na hamasa ikaisha
 
Mmh me nimemsikia tu Huyo Mack Mooger tena bila Alikiba kumuimba nisinge mjua kabisa
 
Ebu dadavua huyo mtu,maana niliona kwenye kitabu cha sugu amemzungumzia kwamba ni msanii ambaye alianza kutoa album kabla yake yeye na pia ali kiba alimuimba huyo msela na ni true story baada ya mshkaji wangu wa m/nyamala kuniambia jamaa mac mooger alikuwepo na alikuwa mtu wa kujirusha sana!!

Aisee ina maana Alikiba alimwimba mtu halisi,nilidhani jina tu la imagination.
Sasa Mr.Nice alikuwa anajishtukia nini!
 
Pompidou alikuwa inafrika band sina hakina kama yupo mpaka leo maana band yenyewe imeshuka kimtindo...

Inafrika Band naona picha zao kwenye mitandao ya jamii, kwa sasa hivi naona wamejikita sana katika kufanya tours za Ulaya na Asia.

Ras Pompidou mzee wa "Kivyakovyako" bado yupo nao.

Kuna wakati katika.mashindano ya "Yo Rap Bonanza" ya marehemu Kim Mgomelo, Pompi alipanda mzuka.kama Shabba akafoka mpaka kupanda juu ya speaker.

Siku nyingine alizingua watu pale IPS Building (sijui linaitwaje siku hizi) nje, wabongo mpaka wanaulizana "huyu ni Mtanzania"?
 
Hata Mimi nilimsikia kupitia nyimbo ya alikiba, nilijaribu kumtengeneza kwa kutumia fikra zangu alikuwa ni mtu wa aina gani na ni nani, kwa kifupi nilitaman kujua hostoria yake kwa ujumla ila nyimbo ilivyokufa na hamasa ikaisha

Mac Mooger alitoa albam yake "The Mac Mooger" kabla ya Mr. II (enzi hizo 2 Proud) na kuiuza kwa muhindi mmoja anaitwa Mamu. Enzi hizo za kina "Weusi Wagumu Asilia". Kabla Steve 2K hajaingia studio Don Bosco kurekodi usiku mzima kutoka Tanga.

Mac Mooger alikuwa anasifika kwa kuwa na pumzi sana halafu akiingia studio anavyorekodi yeye ni one take tu, hamna kurudia rudia. Hakuuza sana kwa sababu ali rap kiingereza sana wakati watu walimuwa wanazibukia Kiswahili.

Sina uhakika kama ni huyu ndiye anaimbwa na Ali Kiba, ila sitashangaa ikiwa hivyo kwani Hip Hop ilikuwa bado hailipi sana siku.zile, na mchizi alivyozibula niaingeshangaa kama alitokomea South kama.alivyoimba Ali Kiba kwa sababu vijana wengi walizibukia kwenda South.
 
Mac Mooger alitoa albam yake "The Mac Mooger" kabla ya Mr. II (enzi hizo 2 Proud) na kuiuza kwa muhindi mmoja anaitwa Mamu. Enzi hizo za kina "Weusi Wagumu Asilia". Kabla Steve 2K hajaingia studio Don Bosco kurekodi usiku mzima kutoka Tanga.

Mac Mooger alikuwa anasifika kwa.kuwa na pumzi sana halafu akiingia studio anavyorekodi yeye ni one take tu, hamna kurudia rudia.

Shukrani
Bado nashauku ya kujua mengi kuhusu huyu jamaa, kama bado yupo au lah
 
Inafrika Band naona picha zao kwenye mitandao ya jamii, kwa sasa hivi naona wamejikita sana katika kufanya tours za Ulaya na Asia.

Ras Pompidou mzee wa "Kivyakovyako" bado yupo nao.
hizi band zinapoenda tour huwa zinapelekwa na nani,maana band ina watu wengi,ukija upande wa kizazi kipya utakuwa msanii anasikika sana ila hizo chance za kwenda nje mara chache sana
 
Oh Jah Kimbute yupo wapi huyo mtu, alikuwa anakula Kida Waziri baada ya kifo cha mzee Maneti wa vijana jazz
 
hizi band zinapoenda tour huwa zinapelekwa na nani,maana band ina watu wengi,ukija upande wa kizazi kipya utakuwa msanii anasikika sana ila hizo chance za kwenda nje mara chache sana

Inafrika ni bendi kongwe imekuwapo kwa zaidi ya miaka 20, ina network kubwa na studio yake (Soundcrafters). Washapiga mahoteli makubwa mengi kuanzia Kilimanjaro mpaka vi pub / club kama "The Place" (pamebadilishwa jina na setup siku hizi. I was there last year sikumbuki panaitwaje, Shoppers Plaza kwa juu hapa).

Ukiwa kwenye network kama hii kwenye mahoteli makubwa, na kama muziki wako ni mzuri, kupata mialiko ya nje si kazi sana.
 
  • Thanks
Reactions: prs
Ukimpata Baba T anaweza kuwa na habari za Jah Kimbuteh
 
Back
Top Bottom