Wako wapi hawa wasanii?

Big up Kiranga kwa info.

Thanks.

I was there when it all went down.

Watu walivyorekodi kuanzia Soundcrafters Temeke, Don Bosco, kwa Master J Oysterbay, Mawingu mpaka kwa P Funk Masaki.

Tangu enzi za Kim Mgomelo na "Yo Rap Bonanza". Mr 2 anatoka Mbeya na kukaribishwa " Dar Young Mob".

Tangu enzi hizo vijana waliokuwa wanapenda kuwa wasanii lazima kupitia sehemu kama Korea Cultural Centre kujifunza kupiga ala na kusoma musical notes.

Tangu enzi za Raiders Posse mpaka Kwanza Unit walivyomzika Adili Kumbuka "Nigger One" makaburi ya Karume pale Ilala nilikuwepo.

Tangu Professor Jay hajaruhusiwa kushika mic Hard Blasters, anaruhusiwa kubandika posters za concerts tu, enzi za "Tough Jam" kabla Tough hajajikata Marekani (mchizi yule angebaki bongo hatari yake ingekuwaje sijui, maana alikuwa ana flow utafikiri ni.member wa "Fu Shnickens" ).
 
Last edited by a moderator:
Reactions: prs
Nasikia hili kundi la Hard Blasters ilivunjika kutokana na baadhi ya members kuzidi kuvuta bangi kitu kilichosababisha Professor J kujitoa huko.

Je ni kweli kwamba hao Kwanza Unit ndo kundi la kwanza la Hip hop kurekodi.
 
Umenikumbusha beach parties za Clouds enzi hizo. More than 20 yrs ago. Damn.
 
Weusi Wagumu Asilia wali rekodi kabla ya Kwanza Unit, Mac Mooger na Mr. 2.
 
Umenikumbusha beach parties za Clouds enzi hizo. More than 20 yrs ago. Damn.

Umenikumbusha moja particularly Mikadi Beach. Bonnie Luv alirusha sana watu. Enzi hiyo ndiyo kwanza Buju katoa "Champion".

Bonnie alikuwa anapenda sana ugomvi wa mitaani Upanga na kudandia mabasi zamani, kuja kustuka yupo on the one and two's nikataka kucheka mchakaramu kawa DJ.

Duh, it's been a minute.
 
Umenikumbusha moja particularly Mikadi Beach. Bonnie Luv alirusha sana watu. Enzi hiyo ndiyo kwanza Buju katoa "Champion".

Duh, it's been a minute.

I know! Sometimes it feels just like yesterday.

Halafu kuna wakati walikuwa wanafanya kama za kustukiza tu hivi. Circle ya watu flani wachache ndo wanajua lakini habari inaenea na mtu zinashona.

Na hapo kabla hata watu hawajawa na cell phones kihivyo kama ilivyo sasa!
 
Kwanza nikusahihishe aliyeimba "eite sevena pointa eite "ni Kiada Man sio Ras Pompidu
Pompi yupo In Africa Band na akina Enrico,Steve RnB na wengineo wanasafiri sana nje kupiga mahotelini
 
Sasa mbona mikoani hawajulikani mpaka leo !

Inategemea unatoka mkoa gani na umezaliwa mwaka gani?hiyo kuuliza tu clouds wameanza fulsa zaman inaonyesha ni dogo so hao ni mali gendary inabidi uwe wa zamani kidogo
 
Inategemea unatoka mkoa gani na umezaliwa mwaka gani?hiyo kuuliza tu clouds wameanza fulsa zaman inaonyesha ni dogo so hao ni mali gendary inabidi uwe wa zamani kidogo
Kwani Clouds walianza lini?
 
Mac Mooger ni dereva tax jamani zaman alikuwa akipaki kinondon soko la Tx sikuwa najua kama ndio huyo aliyeimbwa na Ali kiba alikuwa Dereva tax naemtumia wkt naishi kinondoni kwa sasa sijui yupo wapi ila alinieleza sababu iliyompelekea kushuka mpk kuendesha tax ndipo nikamjua ndo yule aliyeimbwa na Ali kiba ila jaman ktk maisha tukubaliane na hali yoyote ile endapo utaporomoka kifedha
 
Kwanza nikusahihishe aliyeimba "eite sevena pointa eite "ni Kiada Man sio Ras Pompidu
Pompi yupo In Africa Band na akina Enrico,Steve RnB na wengineo wanasafiri sana nje kupiga mahotelini

Yes sir I gotchu my nikka ,its KIADA MAN.
 
Dah enzi za Dar Young Mob, Weusi Wagumu Asili zilikuwa tamu sana..... rap za kwanza kwanza zilizonifurahisha ilikuwa ni pamoja na chuzi limekubali, mabishoo wa bongo na dar young mob. Mambo ya bottle party coco beach su picnic msasani maisha yalikuwa matamuu japokuwa ndo tulikuwa wadogo wadogo hivi. Hivi braza men mmoja alikuwa mkali wa Basketball anaitwa Mpoki alikwua anakaa masaki karibu na mitaa ya vatcan yupo wapi siku hizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…