Wako wapi mabinti waliotajwa na FA kwenye wimbo wa “Mabinti”?

Wako wapi mabinti waliotajwa na FA kwenye wimbo wa “Mabinti”?

Nakumbuka wimbo huu ulifanana Sana na wimbo wa Jay mo Kama unataka demu... Kiasi ikaleta bifu Kati ya wawili hao coz Kila mtu alisema mwenzie kaiba idea...Hadi Leo hatujui idea ilikuwa ya Nani
Upi ulianza kutoka kati ya Jay mo au Mwana fa?
 
Studio ilikuwa Bongo Records au kwa Master J ila kwa P.Funk ndio palikuwa hot aisee!!!
Wana wote lazma wafanye beats bongo records!
Producers wa samani walikuwa na blueprint zao ilikuwa rahisi kumtambua producer kwa beat tu .

Majani

Master j

Amit mento

Miika mwamba

Henrico wa soundcrafters .

Backyard records .
 
True that!

Shule pia ilikuwa muhimu, ndiyo maana unasikia wengine wapo Vodacom sijui Stanbic mara States.... hizi takataka za kileo zinaishia Instagram tu.

“Kuna mabinti wapo kamili kila idara, familia bora na akili zisizolala... maumbo bomba na sura”.
Asilimia kubwa miaka ile shule ilikuwa inazingatiwa sana na wazazi walitilia mkazo kweli kweli.

Ulikuwa unaruhusiwa kufanya mambo yako unayoyapenda kama music au modelling kwa wanawake ila mzazi anakupa masharti lazima ufanye vizuri darasani usimuangushe kwa kuamini. Kwa hiyo wengi walikuwa wanafanya vizuri kila idara.
 
Halima namfaham sikuwahi kujua Kama alitajwa kwenye hii nyimbo, mdogo ake wa kiume kazaa na Rose ndauka mtoto wa kwanza. Alikuwa anafanyakazi Vodacom.
Dogo anaitwa Malik alikuaga na TNG Crew.Dada ake alikuaga poa sana
 
Back
Top Bottom