Pole nyingi kwa waliopoteza ndugu, marafiki na majirani ambao walistahili kuishi lakini shetani na mawakala wao wamewaondosha katika Ulimwengu huu.
Mungu mwenye huruma na mamlaka yasiyo na mipaka tunaomba awapokee marehemu hawa kwenye ufalme wake wa milele ulio na haki isiyo na mashaka. Mungu mfariji atupe faraja watanzania wote tulioguswa na vifo hivi vilivyosababishwa na shetani ambaye tulidhani ni mwanadamu mwenye hofu ya Mungu.
Mungu wetu, kisasi kipo juu ya mamlaka yako lakini maombi yetu ni kuwa laana na damu za marehemu hawa zikakae kwao walioamrisha mauaji, watekelezaji, mawakala wao na wafurahiao mauaji ya wana wako. Wao wanaua kwa mamlaka na kwa bunduki lakini wewe huhitaji bunduki wala rungu, wala fimbo kuweza kuwaadhibu na kuwakumbusha kuwa juu yao kuna mamlaka iliyo kuu ambayo ni Wewe mwenyewe.
Nyumba zao zikadumu katika laana na mateso. Nao wakakumbuke, wakajutie, na mwishowe wakakusujudie kwa matendo na kauli maana nyumba na familia zao hazitapungukiwa mahangaiko na mateso. Nao wasiotubu, damu za marehemu zikawafuate na kuwalilia wakati wote wa maisha yao.
Sent using
Jamii Forums mobile app