Wako wapi Man Dojo na Domokaya?

Wako wapi Man Dojo na Domokaya?

Hawa jamaa hata mimi huwa sichoki kuwasikiliza,nilipenda sana nyimbo zao kipindi kile,mwenye kuweza atuwekee nyimbo zao humu,

Pia wako wapi wale wakali wa kucheza "Disco" enzi zile? Akina Athumani Digadiga,Black Moses na wengineo?

Yuko wapi Saleh Jabir wa Bongo fleva enzi zilee Bongo fleva ndio inaaza?
kaka we acha tuu me nkiwaza mambo yalivyokua matamu naumia kinoma yani, liko wapi kundi la EAST COST TEAM?
 
Daaaah leo niliwakumbuka sana maana nimeisikia ngoma yao ya Dingi ikipigwa redioni,jamaa walikuwa wakali sana.
 
Daaaah leo niliwakumbuka sana maana nimeisikia ngoma yao ya Dingi ikipigwa redioni,jamaa walikuwa wakali sana.
me na uhakika dingi ikiwekwa kwenye chat tena sokoni itavunja record ya mauzo.
 
muda mwingine mziki ni swaga za utotoni tuu mtu akikua anaacha....game lenyewe hili hutoki mpaka umezeshwe kete za ngada
Ni kweli unachokisema lakini hawa jamaa walifanya kweli kiasi cha jamii kuwakubali, tatizo la mziki wa sasa ni copy and paste, hakuna ubunifu ndani yake. Mbona mrisho mpoto anatusua?
 
Back
Top Bottom