Wako wapi mapedeshee walioimbwa na kugawa pesa kwa wasanii wa bendi?

Nakumbuka kufuru aliyofanya Ndama mtoto wa ng'ombe kwa Fary Ipupa hadi Ipupa akapagawa kidogo amsahau jidada bonge Yasmine ,kumbe ni hela ya sembe,sijui kesi yake ya kutakatisha pesa ya sembe imeishia wapi.
 
Kuna pedeshee mwingine a.k.a fisadi Lowasa, alikuwa mpaka anadekiwa barabara ndo apite, naye kayeyuka pia!
Kwa mara ya mwisho alionekana akipanda daladala ya Gongo la Mboto kwenda Posta baada ya matumaini kuishia Sheikh Amri Abeid,ila akina Musukuma,Lugola,Tibaijuka ni watu wabaya sana wamemuacha mwenzao solemba mchana kweupe pee
 
Hahaaaaaaaaa
 
Powder zimewekewa mkazo hawapenyezi ki rahisi
Pedeshee kifaranga totoo ya kuku
 
Kwa mara ya mwisho alionekana akipanda daladala ya Gongo la Mboto kwenda Posta baada ya matumaini kuishia Sheikh Amri Abeid,ila akina Musukuma,Lugola,Tibaijuka ni watu wabaya sana wamemuacha mwenzao solemba mchana kweupe pee
[emoji3] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji3] jamaniiii!!
 
[emoji2] [emoji2] [emoji57] [emoji3] [emoji3] [emoji57]
 
Ndama Mutoto ya ng'ombe
Chicago Matelefoni
Papaa Musofe
Chief Kiumbe
Na wengine wako Wapi?
Tumewamiss sana, hata muziki wa bendi umedorora kwa ukimya wenu
Hivi huyo chief Kiumbe ndo yule mtaalam wa karate na judo au?
 
Naelekea lusaka kwenye onyesho la Koffie Olomide , hii nchi yenu yenye majonzi siku zote nawaachieni kwa muda .

Bendi zote zimekufa kwa ukata uliotokana na dhiki kubwa iliyolikumba Taifa , imebaki police jazz band tu wana vangavanga
 
Unaenda kuangalia onyesha la mpiga mateke wanawake halafu kesho ndio uje upande majukwaani eti ni muokozi wa wanawake,buure kabisa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…