Wako wapi wachezaji hawa wa zamni wa Simba na Yanga?

Daaa safi sana nimejua mambo mengi toka kwa mafundi wa zamani inaoneka mpira wa zamani ulikua mtamu sana
Edward chumila aka eddo ningependa kumjua jamani au george magele masatu
 
Yuko wapi Lulanga Mapunda? Chibe Chibindu? Kipanya Malapa? Quresh Ufunguo? Shengo Tondola? John Masamaki?
 
.......Na ilipelekea wachezaji wa Yanga kugoma kule Mombasa kwenye klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati nafikiri ilikuwa mwaka 1984 wakidai acheze Elisha John.
Nakumbuka Elisha alipewa na Yanga shilingi laki moja 1983 wakati anatoka Simba, ilikuwa hela nyingi sana wakati ule. Baadaye Elisha baada ya mambo kumuwia vigumu Yanga aliamua kutimkia Uarabuni.
 
Upo sahihi kabisa mkuu. Tena mashindano yale Yanga ilikua iko vizuri sana maana walianza kwa kuwachapa mabingwa wa Zambia wakati huo Nkana Red Devils bao 2-0

Kama sio mgogoro ule Wananchi wangeweza kutoroka na kombe lile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…