Wako wapi wachezaji hawa wa zamni wa Simba na Yanga?

Wako wapi wachezaji hawa wa zamni wa Simba na Yanga?

Daaa safi sana nimejua mambo mengi toka kwa mafundi wa zamani inaoneka mpira wa zamani ulikua mtamu sana
Edward chumila aka eddo ningependa kumjua jamani au george magele masatu
 
Yuko wapi Lulanga Mapunda? Chibe Chibindu? Kipanya Malapa? Quresh Ufunguo? Shengo Tondola? John Masamaki?
 
Aamin. Ingawa hawa wachezaji walicheza katika vipindi viwili tofauti. Wakati Yanga Fadhili Bwanga alivuma miaka ya 1970s akiwa Dar Young Africans, Elisha John alitingisha miaka ya mwanzo ya 1980s akitokea Coastal Union kwenda Simba SC kisha Young Africans

Usajili wa Elisha John kutoka Simba kwenda Yanga ulivunja rekodi ya fedha ya uhamisho pamoja na kwamba soka lilikuwa la ridhaa wakati huo huku akiwa analipwa mshahara mnono tofauti na wenzie kitendo kilicholeta mtafaruku kwenye timu ikiwepo kuletwa mgomo baridi miongoni mwa wachezaji wengine
.......Na ilipelekea wachezaji wa Yanga kugoma kule Mombasa kwenye klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati nafikiri ilikuwa mwaka 1984 wakidai acheze Elisha John.
Nakumbuka Elisha alipewa na Yanga shilingi laki moja 1983 wakati anatoka Simba, ilikuwa hela nyingi sana wakati ule. Baadaye Elisha baada ya mambo kumuwia vigumu Yanga aliamua kutimkia Uarabuni.
 
Upo sahihi kabisa mkuu. Tena mashindano yale Yanga ilikua iko vizuri sana maana walianza kwa kuwachapa mabingwa wa Zambia wakati huo Nkana Red Devils bao 2-0

Kama sio mgogoro ule Wananchi wangeweza kutoroka na kombe lile
 
Back
Top Bottom