Wako wapi wakuamini vijana

Wako wapi wakuamini vijana

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
ATI HATUJIELEWI

Hatujishughulishi
Na mnatujaji
Hatuna mitaji
Nyie wafujaji
Manayajaza matumbo yenu

Mtumba mitumbani
Tunalipa kodi
Bila ukaidi
Nyie mwafaidi
Mazingira yetu bado duni

Shamba ni mkombozi
Mbolea zauzwa
Mbegu zinauzwa
Maji yanauzwa
Bila pesa hakuna mavuno

Ajira ni kubeti
1 kwa milioni
Tv, redioni
Bar,hotelini
Faida kubwa wapata wao

Mapenzi ya kisasa
Ndio biashara
Kunayo hasara
Hakuna busara
Nayo yatukidhi mahitaji

Abuuabdillah ✍️🇹🇿
0718569091
Kilimanjaro
 
Back
Top Bottom