Formal education kazi yake ni kutufunua akili tuyajue mazingira na tujue jinsi ya kuyaendesha hayo mazingira,ila haihusiani na formula za kutafuta pesa aisee.Maisha ni mwalimu mzuri.Kuna Ile tabia mtu anakaribia kumaliza chuo au anakuwa amemaliza kabisa chuo anakuwa anapanga kabisa kwamba Mimi nikienda mtaani sifanyi kazi chini ya hela kiasi Fulani.
Watu wanajipangia mishara mikubwa sana na kujiaminisha.Wakija kuingia na mtaani Kwanza wanakutana na ukosefu wa ajira, kwahiyo wanabaki kusugua benchi nyumbani.Baadaye mtu ana learn the hard way.Na mwisho wa siku akipata hata tenda ya Kiasi kadhaa(kidogo) unakuta anakimbilia haraka Sana na kuona hili nalo embe dodo mchangani.
Achaneni kabisa.
Formula za kutafuta pesa zipo kitaani/informal education.
Pia tatizo elimu yetu imejengeka kutujaza fikra toka tuko shule kuwa soma upate ajira uishi maisha mazuri kwa mshahara mzuri.
Hata walimu mashuleni wasikilize utasikia wakibwatuka hivyo"someni muwe madaktari ama wahandisi mpate mishahara mikubwa muishi maisha mazuri".
Kumbe katika ajira kuna ushindani pia.