Wako wapi wale wasabato wa zamani?

Wako wapi wale wasabato wa zamani?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Nimetoka mkoa wa Mara-Tanzania, sehemu niliyokulia Mimi Kuna wasabato wengi kiasi, Pamoja na dhehebu la menonite ndio wamedominate huko. Kwenye familia yetu mzee wangu sio msabato, Lakini kaka zake na ndugu kiasi ni wasabato. (Mzee wangu alioa wanawake wawili) ni kama Hana tu dini.

Nilipokua naenda kwa baba mkubwa wangu (miaka ile) ukifika unajua fika kabisa hapa nipo kwa wasabato waishikao siku ya saba, nikimaanisha ikifika Jumamosi hakuna kazi yoyote kufanyika, kama ni chakula kinapikwa ijumaa, Jumamosi ni kanisani kuanzia asubuhi mpaka jioni, kwaya zinazopigwa ni kurasini, Muungano,sauti ya jagwani, mkendo,iringo na bubombi. Hawakuitambua sikukuu za kimataifa, ujichanganye uende kwa baba mkubwa Christmas andika maumivu ni ugali na dagaa.

Nilipoenda advance kipindi Cha dini nilikua najichanganya kwa wasabato maana siku ya Jumamosi tukienda kanisani washiriki walikua wanatuchukua tunaenda kupiga diko la maana.

Nilipoenda chuo nikakutana na wasabato pia waligomea kufanya mtihani siku ya Jumamosi wakashikilia MSIMAMO wakafukuzwa chuo, wasabato wale ambao ukimtongoza kukubaliwa mpaka uende kwao.

But wasabato wa kipindi hiki hizi sikukuu na wao wamo, Sio Christmas Wala pasaka nao wanasherekea tu hawajui hata vitabu vya Hellen G White, walevi na wengine wanakula mdudu,

Wako wapi wasabato wa kipindi like?
 
Wewe ni dini gani?
 
preview.mp4.jpg
 
Back
Top Bottom