Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi kwa kazi hiyo tena wakaenda mbali kuwa haiko huru tume hiyo kufanya kazi wanayotakiwa kufanya. Sasa baada ya rasimu hii natamani kuwasikia tena wakisema nakurudia maneno yale na pengine kwa kuyapigia mstari mkubwa!!
Nape Nnauye ukitumia akili utajitendea haki, uhuru wa kuiandika hii katiba tumenyimwa,
1) sheria iko wazi inatutishia kupinga muundo wa mchakato wa kuiandika katiba hata kama umekosewa, (hapo uhuru unatoka wapi)
2) vyama vya siasa vinasikilizwa kanakwamba navyo ni wananchi (hiki ni kioja)
3) viongozi wanasikilizwa na tume si kwa utanzania wao, bali kwa nyadhifa zao (hii ni balaa)
Nape kumbuka kuwa vimabadiliko vichache vinavyojitokeza kwenye hii rasimu ya katiba vingeweza kufanywa kwa kupeleka miswada bungeni na kurekebisha katiba hii hii tuliyonayo, kama unaweza kusoma katikati ya mistari utagundua kuwa rasimu ya katiba ya sasa "INAPENDEKEZA MAMLAKA NYINGINE KUFANYA MAAMUZI KWA KADRI ZITAONA INAFAA"
rasimu haielekezi, nieleweke vizuri.
katiba gani inaacha mianya ya rasilimali kuporwa kwa maamuzi ya watu wachache?
katiba gani isiyotambua kuwa maliasili zilizopo nchini kwetu ni zetu 100% na ikiwa hatuna taaluma ya kuzichakata tuweze kumuajiri awezaye kwa percent elekezi i.e up to 30% muximum?
hii katiba ilipaswa kuvielekeza vyama majukumu yao, lakini ajabu vyama vinajipangia vitaendeshaje shughuli zake kiulainiiii hata kama ni kwa hasara ya nchi.
IKIPITISHWA HII KATIBA KWA KWELI HII SI YA WANANCHI WA TANZANIA.